NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amemuagiza Mkurugenzi wa Bonde la Rufiji kukutana na kuzungumza na wananchi wanaomiliki maeneo yaliyo nje ya mita 60 kwenye bwawa la Masaka lilipo Mkoani Iringa. Mahundi ametoa maagizo hayo akiwa kwenye muendelezo wa ziara Mkoani humo na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira leo Machi 14 2024 ambapo kamati imetembelea na kukagua ujenzi wa bwawa hilo la Masaka. Akiwa katika ziara hiyo Mhandisi Mahundi pamoja na kamati wameweza kutembelea ujenzi wa bwawa hilo na kuzungumza na wananchi wa vijiji vya Sadani, Makota na Kaning’ombe ambao ni wanufaika wa bwawa hilo lililojengwa na Wizara ya Maji kupitia Bodi ya Maji Bonde la Rufiji.
“Bwawa hilo litakua na msaada mkubwa katika upatikanaji wa maji majumbani, maji kwaajili ya kilimo, uvuvi pamoja na utalii hivyo nikuagize Mkurugenzi wa bonde la Rufiji uweze kurudi kuzungumza na wananchi hawa wamiliki ambao maeneo yao yapo nje ya mita 60” Akiwasilisha taarifa ya Ujenzi wa bwawa hilo Mkurugenzi wa Rasilimali maji Dkt. George Lugomela ameelezea kuwa litasaidia kuongeza upatikanaji wa rasilimali za maji kwa matumizi ya nyumbani, mifugo, kilimo cha umwagiliaji na Uvuvi.
NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amemuagiza Mkurugenzi wa Bonde la Rufiji kukutana na kuzungumza na wananchi wanaomiliki maeneo yaliyo nje ya mita 60 kwenye bwawa la Masaka lilipo Mkoani Iringa.
Mahundi ametoa maagizo hayo akiwa kwenye muendelezo wa ziara Mkoani humo na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira leo Machi 14 2024 ambapo kamati imetembelea na kukagua ujenzi wa bwawa hilo la Masaka.
Akiwa katika ziara hiyo Mhandisi Mahundi pamoja na kamati wameweza kutembelea ujenzi wa bwawa hilo na kuzungumza na wananchi wa vijiji vya Sadani, Makota na Kaning’ombe ambao ni wanufaika wa bwawa hilo lililojengwa na Wizara ya Maji kupitia Bodi ya Maji Bonde la Rufiji.
“Bwawa hilo litakua na msaada mkubwa katika upatikanaji wa maji majumbani, maji kwaajili ya kilimo, uvuvi pamoja na utalii hivyo nikuagize Mkurugenzi wa bonde la Rufiji uweze kurudi kuzungumza na wananchi hawa wamiliki ambao maeneo yao yapo nje ya mita 60”
Akiwasilisha taarifa ya Ujenzi wa bwawa hilo Mkurugenzi wa Rasilimali maji Dkt. George Lugomela ameelezea kuwa litasaidia kuongeza upatikanaji wa rasilimali za maji kwa matumizi ya nyumbani, mifugo, kilimo cha umwagiliaji na Uvuvi.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.Jackson Kiswaga(Mb) ameagiza chanzo cha bwawa hilo kijengewe miundombinu ya kusambaza ili lianze kutumika,na kuwataka liwekewe mipaka ili kuepuka kuingiliwa na shughuli za wananchi
Bwawa la Masaka ni Bwawa lililojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, kata ya Masaka yenye vijiji vitatu ambapo ujenzi wa bwawa hilo umetekelezwa na wataalam wa ndani (Force Account) na umegharimu shilingi bilioni 1.69 na kukamilika kwa mradi huo kutasaidia upatikanaji wa maji kwa vijiji hivyo ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa havina maji ya uhakika .
Mwisho
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.Jackson Kiswaga(Mb) ameagiza chanzo cha bwawa hilo kijengewe miundombinu ya kusambaza ili lianze kutumika,na kuwataka liwekewe mipaka ili kuepuka kuingiliwa na shughuli