Mwenyekiti wa Wanawake Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya Aminael Julias ameongoza wanawake wenzie kutoa faraja Kambi shule ya msingi Tambuka reli Kata ya Itezi Jijini Mbeya kwa waathirika wa maporomoko mlima Kawetere yalitokea aprili 14,2024.Aminael amesema wao kama Wanawake wameguswa na tukio hilo zito hivyo wamekabidhi nguo za kike,taulo za kike,pampas,vyakula na mipira kwa ajili ya kuchezea watoto.
Mwakilishi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa amewashukuru Wanawake hao kwa namna walivyoguswa kutoa msaada kwani serikali peke yake isingeweza kukabiliana na tatizo hilo hasa ikizingatiwa baadhi ya waathirika hawakuweza kuokoa chochote katika nyumba zao.
Ziara hiyo iliongozwa na Afisa Uhisiano Neema Stanton.
Mwenyekiti wa Wanawake Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya Aminael Julias ameongoza wanawake wenzie kutoa faraja Kambi shule ya msingi Tambuka reli Kata ya Itezi Jijini Mbeya kwa waathirika wa maporomoko mlima Kawetere yalitokea aprili 14,2024.
Aminael amesema wao kama Wanawake wameguswa na tukio hilo zito hivyo wamekabidhi nguo za kike,taulo za kike,pampas,vyakula na mipira kwa ajili ya kuchezea watoto.