Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

ONYO KALI KWA VIBAKA KUTOKA KWA WAMACHINGA SOKO LA JIONI KABWE JIJI LA MBEYA VIBAKA NA WEZI WAUFYATA

July 6, 2025

MNEC: MWASELELA ASIMAMISHA MINONG’ONO YA KISIASA MBEYA MJINI

July 3, 2025

KWA MARA NYINGINE, MHANDISI MAHUNDI AWAPA NEEMA WAGONJWA WA MACHO

July 1, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • ONYO KALI KWA VIBAKA KUTOKA KWA WAMACHINGA SOKO LA JIONI KABWE JIJI LA MBEYA VIBAKA NA WEZI WAUFYATA
  • MNEC: MWASELELA ASIMAMISHA MINONG’ONO YA KISIASA MBEYA MJINI
  • KWA MARA NYINGINE, MHANDISI MAHUNDI AWAPA NEEMA WAGONJWA WA MACHO
  • MWAKIPESILE AREJESHA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI
  • Msimu wa pili wa tamasha la michezo na vipaji MZRH
  • MKULIMA NA MFUGAJI WA MBARALI ATIA TIMU KIPUTE JIMBO LA MBARALI USANGU ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE
  • WAKILI MSOMI KAPTENI MSTAAFU SAMBWEE SHITAMBALA ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI.
  • MWAISUMBE: ALIYEJITOSA UBUNGE 2010 AWANIA TENA MBEYA MJINI AAHIDI KUMUUNGA MKONO ATAKAYETEULIWA
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » RAIS SAMIA HATAKI MISUKOSUKO KWA WAFANYABIASHARA- DKT. BITEKO
Habari za Kitaifa

RAIS SAMIA HATAKI MISUKOSUKO KWA WAFANYABIASHARA- DKT. BITEKO

Mbeya YetuBy Mbeya YetuMarch 10, 2024Updated:March 10, 20241 Comment6 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amejipambanua kama mlezi wa Sekta binafsi nchini na hataki kuona wafanyabiashara wanapata misukosuko wakati wa utekelezaji wa majukumu Amesema maono ya Rais ni kujenga sekta binafsi itakayokuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye pato la Taifa na ili kufikia azma hiyo, viongozi wengine wahakikishe nia njema ya Rais kwa Wafanyabiashara inatekelezwa kwa vitendo.Amesema maono ya Rais ni kujenga sekta binafsi itakayokuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye pato la Taifa na ili kufikia azma hiyo, viongozi wengine wahakikishe nia njema ya Rais kwa Wafanyabiashara inatekelezwa kwa vitendo.

📌 Ataka Watendaji Warasimu wajionee aibu;watimize wajibu

📌 Watumishi wakumbushwa shughuli za Serikali kufanyika Dodoma

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amejipambanua kama mlezi wa Sekta binafsi nchini na hataki kuona wafanyabiashara wanapata misukosuko wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Amesema maono ya Rais ni kujenga sekta binafsi itakayokuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye pato la Taifa na ili kufikia azma hiyo, viongozi wengine wahakikishe nia njema ya Rais kwa Wafanyabiashara inatekelezwa kwa vitendo.

Dkt. Biteko amesema hayo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Rafiki Hoteli ambao ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda.

Aidha, Dkt. Biteko amewaagiza watendaji wa Serikali kuhakikisha wanailea Sekta binafsi na kila mtu atimize wajibu wake kwenye eneo lake “kama wewe ni Afisa wa TANESCO uliye na wajibu wa kumuunganishia mfanyabiashara umeme ambao mwisho wa siku ataulipia kwa ajili ya mapato yako, huna sababu ya kumwambia njoo kesho wakati kazi hiyo ungeifanya leo.”

Amesema Watendaji ambao ni warasimu lazima waone aibu kwa kuchelewesha shughuli zinazoijenga nchi.

Dkt. Biteko amesema kuwa, Rais, Dkt. Samia anataka kuona watanzania wakiwa kwenye daraja la kwanza katika nchi yao na pia waweze kufanya uwekezaji ndani na nje ya nchi bila vikwazo vyovyote.

Kuhusu Sekta ya Utalii nchini, amesema bado kuna changamoto ya upungufu wa vitanda kwa wageni wa ndani na nje ya nchi hivyo bado kuna kazi kubwa ya kuwekeza kwenye sekta ya hospitality ambapo amewapongeza wamiliki wa Rafiki hoteli na wawekezaji wengine ambao wanaifanyia kazi changamoto hiyo.

Vilevile, Dkt. Biteko ameipongeza menejimenti ya hoteli hiyo kwa kutekeleza dhana ya nishati safi ya kupikia kutokana na kuweka miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwenye hoteli husika na kutoa wito kwa wananchi kutoharibu mazingira na kutokukata miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesisitiza umuhimu Idara na taasisi mbalimbali Serikalini kutumia miundombinu ya uwekezaji Jijini Dodoma ambayo ndio Makao Makuu ya Nchi.

Kutokana na hilo ameagiza Watendaji wa Serikali kuhakikisha kwamba shughuli zinazoweza kufanyika ndani ya Mkoa wa Dodoma zifanyike katika Mkoa husika ili pia kutoa fursa kwa wanachi kupata huduma muda wote pale wanapohitaji huduma za watendaji hao.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu na Mmiliki wa Rafiki Hoteli Fladmiry Mallya ameishukuru Serikali kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji ambayo yanafanya Watanzania kuendelea kuwekeza kwenye nchi yao na hivyo kuwa na mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi na kukuza ajira.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

MHASIBU SUA AJITOSA UBUNGE JIMBO LA SAME MASHARIKI

June 28, 2025

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO WANOLEWA

June 22, 2025

VIJANA CCM MBEYA DC WAJIPANGA KUPIGA KURA OKTOBA 2025.

June 13, 2025

1 Comment

  1. Doncaster escorts on January 22, 2025 6:26 am

    What’s Happening i am new to this, I stumbled upon this I’ve discovered It absolutely helpful and it has helped me out
    loads. I’m hoping to give a contribution & help different customers like its helped me.

    Good job.

    Reply

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024173

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202482

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202569

DKT. TULIA ATOA MSAADA WA VIPAZA SAUTI MSIKITI WA MASJID BI FATMA NZOVWE JIJINI MBEYA

March 29, 202460
Don't Miss
Video Mpya

ONYO KALI KWA VIBAKA KUTOKA KWA WAMACHINGA SOKO LA JIONI KABWE JIJI LA MBEYA VIBAKA NA WEZI WAUFYATA

By Mbeya YetuJuly 6, 20250

#mbeyayetutv

MNEC: MWASELELA ASIMAMISHA MINONG’ONO YA KISIASA MBEYA MJINI

July 3, 2025

KWA MARA NYINGINE, MHANDISI MAHUNDI AWAPA NEEMA WAGONJWA WA MACHO

July 1, 2025

MWAKIPESILE AREJESHA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI

June 30, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

ONYO KALI KWA VIBAKA KUTOKA KWA WAMACHINGA SOKO LA JIONI KABWE JIJI LA MBEYA VIBAKA NA WEZI WAUFYATA

July 6, 2025

MNEC: MWASELELA ASIMAMISHA MINONG’ONO YA KISIASA MBEYA MJINI

July 3, 2025

KWA MARA NYINGINE, MHANDISI MAHUNDI AWAPA NEEMA WAGONJWA WA MACHO

July 1, 2025
Most Popular

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024173

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202482

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202569
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.