Wananchi wa kata ya Nzovwe na Mabatini jijini Mbeya wameiomba serikali kuwalipa fidia ya kuwasimamisha uendelezaji wa makazi yao na shughuli nyingine za kiuchumi kwa zaidi ya miaka kumi na mbili baada ya mabadiliko ya sheria ya hifadhi za barabara ya kuongeza mita saba mbele kutoka mita 22.5 za awali.
Wananchi wamepaza kilio hicho kwa serikali na kuiomba kuwalipa fidia baada ya kuwakataza kuendeleza makazi yao kwa ajiri ya hifadhi ya barabara ambapo wamedai walifanyiwa tathimini ya nyumba zao toka mwaka 2012 na kwa sasa hawana matumaini ya kulipwa kutokana na mabadiliko yaliyojitokeza.
Timu ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Patrick Mwalunenge kwa kushrikiana na ofisi ya Meneja wa TANROADs mkoa wa Mbeya wamefika eneo lenye mgogoro ili kujionea hali halisi na maelekezo ya chama kwa wananchi.