Browsing: Video Mpya

Mratibu wa Kambi ya Madktari bingwa wa rais samia kutoka wizara ya afya Bi. Jackline Ndeshau ameeleza kuwa wamejipanga kuhudumia wananchi wote watakaojitokeza kipindi cha siku 5 za kambi hii mkoani songwe katika maeneo 5 na kutoa rai kwa wananchi kujitokeza kutumia fursa hiyo ambapo lengo lake ni kusogeza huduma za afya karibu na jamii, kuongezea ujuzi wataalamu wa afya waliopo katika vituo husika vilevile kupunguza gharama za kwa wananchi kuzifwata huduma hizo za kibingwa nje ya kituo husika.
Amesema kambi ya madaktari bingwa na bobezi wa Rais Samia wanategemea kutoa huduma za afya kwa watoto na watoto wachanga, huduma za upasuaji, huduma za afya ya uzazi, wajawazito na magonjwa ya wanawake, huduma za ganzi na usingizi na huduma ya magonjwa ya ndani mkoani songwe kwa siku tano katika hospitali za wilaya ya Tunduma, Itumba, Vwawa, Momba na hospitali ya halmashauri wilaya ya Songwe

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprica Mahundi (Mb) amesema Serikali inatarajia kujenga jumla ya minara 15 katika kata mbalimbali za Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Naibu Waziri Maryprisca amesema hayo tarehe 13 Mei, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Isseke, Wilaya ya Manyoni akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa mnara wa mawasiliano unaojengwa na kampuni ya simu ya Airtel kwa kushirikiana na UCSAF.
Amesema minara hiyo 15 itajengwa katika kata za Isseke, Makanda, Makutupora, Maweni, Mitundu, Mkwese, Mwamagembe, Nkonko, Rungwa, Sanjaranda, Sanza, Saranda, Sasajila na Sasilo ili kuimarisha huduma za mawasiliano.
Akizungumzia Mnara wa Isseke unaoendelea na ujenzi,
Mhandisi Maryprisca amesema umeigharimu Serikali jumla ya
Tsh. 116,500,000/- ambapo asilimia 70 ya fedha hizo ambazo ni Tsh. 81,550,000/- tayari zimeshalipwa na UCSAF kwa Airtel.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa mara huo na kuanza kutoa huduma ya Mawasiliano kutawasaidia wakazi wa Vijiji vitakavyofikiwa kwa kuboresha shughuli za kiuchumi na
kupata mawasiliano kwa haraka hususan taarifa muhimu za masoko.
Amesema mawasiliano ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi wa Manyoni kwani yatasaidia pia kuokoa muda wa kufunga safari ili kupata huduma umbali mrefu na kurahisisha huduma za kutuma na kupokea pesa ambazo sasa zitatanyika majumbani.

“Tunaishukuru sana kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na UCSAF, kwa kuchukua uamuzi huu wa kuipa
Wilaya ya Manyoni kipaumbele na kuamua kufikisha huduma za mawasiliano ya uhakika kwa wakazi zaidi ya 6,900 wa vijiji
Maryprisca.