Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya CPA Gilbert Kayange amesema Mamlaka yake ina dhamana ya kutoa huduma ya maji Safi na Usafi wa Mazingira kwa wananchi wanaoshi Jiji la Mbeya na Mji wa Mbalizi.
Katika kutoa huduma za maji safi na usafi wa mazingira mamlaka inazingatia malengo yake na Taifa mwaka 2020 kuwa ifikapo mwaka 2025 kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)kuhakikisha huduma za maji zinapatikana kwa asilimia 95.
Ameyasema hayo baada ya kutembelea maendeleo ya ujenzi wa tanki mradi mkubwa wa kimkakati Kiwira linalojengwa Forest mpya Jijini Mbeya.
CPA Kayange amefurafishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwezi machi 31,2025 uwe umekamilika.
Aidha ametaka ushirikiano baina ya Mamlaka, Mhandisi Mshauri na Mkandarasi kuhakikisha kazi inafanyika Kwa Kasi na ubora unaotakiwa.
Kwa upande wake Mhandisi Barnabas Konga msimamizi wa mradi huo amesema usanifu wa mradi umekamilika ambapo utatakelezwa kwa kipindi cha miaka miwili na kwamba mradi utakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.
Naye Mhandisi Colman Ngainayo Mshauri katika mradi huo amesema vifaa vingi vimesogezwa eneo la mradi na kazi itakwenda kwa kasi kama ilivyokusudiwa.
Naye Mhandisi msaidizi Hendrick Munuo Mkandarasi anayetekeleza mradi huo amesema kwa sasa mradi unatekelezwa kwenye banio,tanki la kusafishia maji na tanki lenye uwezo wa kupokea lita milioni tano za maji lililopo Forest mpya Jijini Mbeya ambapo kazi zote hizo zinakwenda vizuri.
Kukamilika kwa mradi wa maji Kiwira mbali ya Mamlaka kuongeza mapato utamaliza kabisa changamoto ya maji Jijini Mbeya na Wilaya jirani.