Benki ya Maendeleo(TIB) imekabidhi Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya(MBEYAUWSA) hundi ya Mkopo kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ya maji Jijini Mbeya na Mji Mdogo wa Mbalizi.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika Jijini Mbeya ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa ambaye ameitaka Benki kuwekeza zaidi zaidi Mkoani Mbeya kutokana na fursa nyingi zilizopo pia akiishukuru kutoa mkopo kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya TIB Lilian Mbasi amesema Kanda ya Nyanda za Juu Benki imewekeza zaidi ya shilingi bilioni sitini na Mkoa wa Mbeya ukiwa ni moja ya Mikoa iliyonufaika na mikopo.
Naye Zewena Hemed Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miradi anaeleza lengo la mkutano huo kuwa ni kueleza fursa mbalimbali zinazopatikana Benki ya TIB.
Aidha Mjumbe wa Bodi kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya(MBEYAUWSA)Hilda Ngoye amesema mkopo walioupata watautumia kama ilivyokusudiwa.
Baadhi ya Wadau wa mkutano huo wamepata fursa ya kutoa neno akiwepo Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya CPA Chiwanga na Mfanya biashara Machemba.
Benki ya TIB imekuwa ikitoa mikopo yenye riba nafuu kwa wafanyabiashara,wakulima,viwanda na Taasisi za kifedha nchini.