Maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani Mkoa wa Njombe yamefikia kilele kilele chake katika Kijiji cha ltengelo Kata ya Saja Wilaya ya Wanging’ombe Mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka.
Katika hotuba yake Mtaka amewataka wananchi kuungana na Rais katika jitihada za kutunza Mazingira kwa kupanda miti ya matunda na vivuli sanjari na kutunza vyanzo vya maji.
Aidha Mtaka amewataka wananchi kujikita zaidi kupanda miti ya matunda kama parachi na apple ambayo itawawezesha wananchi kutunza Mazingira na kujikwamua kiuchumi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Judica Omary amesema zoezi la upandaji miti Maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani Mkoa wa Njombe yamefikia kilele kilele chake katika Kijiji cha ltengelo Kata ya Saja Wilaya ya Wanging’ombe Mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka.
Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira(NEMC)Kanda ya Nyanda za juu kusini inayojumuisha Mikoa ya Mbeya,Njombe, Songwe na Rukwa Josiah Murunya amesema lengo la kufanya maadhimisho hayo ni kuhimiza zoezi la upandaji miti katika maeneo yote ya Nyanda za juu kusini ili kurejesha uoto wa asili na kutunza vyanzo vya maji ili kuongeza upatikanaji wa maji nchini Mkoa wa Njombe ni endelevu ili kuepukana na jangwa.
Katibu Tawala Wilaya ya Wanging’ombe Veronica Gerald amesema tangu kuanza kampeni hoi zaidi ya miche elfu tatu imepandwa na katika Kijiji cha ltengelo miche elfu moja imepandwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wanging’ombe Agnetha Mpangile amesema zoezi hilo litafanyika katika vijiji vyote ili kuepukana na na jangwa.
Andrew Mangula ni Diwani wa Kata ya Saja na Aidan Mangula Mwenyekiti wa Kijiji wameahidi kuitunza miti hiyo il iweze kuwanufaisha kwa kufuga nyuki na samaki ili kuwaongezea kipato.
NEMC kanda imeendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuwajengea uwezo waweze kujua athari za uharibifu na utunzaji wa mazingira.