Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji (Rufaa), Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mkutano wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Juni, 2024 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari. (Picha na INEC).
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji (Rufaa), Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mkutano wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Juni, 2024 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari. (Picha na INEC).
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K wa mkutano wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Juni, 2024 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari. (Picha na INEC).
Viongozi na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa wakishiriki katika mkutano huo.
Viongozi na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa wakishiriki katika mkutano huo.
Viongozi na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa wakishiriki katika mkutano huo.
Vyama vya
siasa vitaruhusiwa kuweka wakala mmoja kwenye kila kituo cha kuandikisha wapiga
kura kwenye uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotarajiwa
kuzinduliwa mkoani Kigoma, tarehe 01 Julai, 2024.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji
(Rufaa), Jacobs Mwambegele wakati akifungua mkutano wa Tume na viongozi wa
vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Juni, 2024 ikiwa
ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari.
“Leo kila
chama kitapewa nakala ya orodha ya vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura.
Dhumuni la kuwapatia nakala hizo ni kuwawezesha kupanga na kuweka mawakala wa
uandikishaji katika vituo vya kuandikisha wapiga kura,” amesema na kuongeza….
“Kila
chama kitaruhusiwa kuweka wakala mmoja kwenye kituo cha kuandikisha wapiga kura
kwa lengo la kushuhudia utekelezaji wa zoezi la uboreshaji kituoni ikiwemo
kuwatambua wale wanaokuja kituoni kama wana sifa za kuandikishwa”.
Jaji
Mwambegele amesema kwamba kikao hicho ni sehemu ya utamaduni wa Tume
iliojiwekea wa kuwashirikisha wadau wa uchaguzi wakati wa utekelezaji wa
majukumu yake.
Aliwataja
wadau hao kuwa ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa,
Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya
habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi
wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu na wanawake.
” Niwaombe Viongozi wa Vyama vya Siasa kwa umoja wenu kuzingatia
sheria za uchaguzi, kanuni za uboreshaji na maelekezo ya Tume kuhusu zoezi la
uboreshaji wa Daftari. Tume kwa upande wetu tutazingatia Katiba, sheria ya
uchaguzi na kanuni zilizotungwa chini ya sheria katika zoezi hili la
uboreshaji,” amesema.
Kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru
ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K amesema kuwa pamoja na kufanyika kwa
uzinduzi tarehe 01 Julai, 2024 mkoani Kigoma ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa
kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (MB), uboreshaji wa Daftrai
utaanza siku hiyo mkoani kigoma na kuendelea kwa siku saba hadi tarehe 07
Julai, 2024.
”Kwa lengo la kutekeleza jukumu
hilo kwa ufanisi, uboreshaji utafanyika kwenye mizunguko 13 itakayobainishwa
kwenye ratiba. Aidha, zoezi hili litaendeshwa kwa siku saba kwenye kila kituo
cha kuandikisha wapiga kura,” amesema.