Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Sayansi za Afya cha K’s Royal imepata nafasi ya kipekee ya kupongeza uongozi na wafanyakazi wa chuo kwa juhudi zao za kuhakikisha wanafunzi wanapata maarifa na ujuzi wa kisasa ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira nchini. Katika kikao cha hivi karibuni, bodi hiyo ilibaini kwamba chuo kimejizatiti katika kuimarisha mitaala na mafunzo ambayo yanajibu moja kwa moja changamoto zinazokabili sekta ya afya nchini.
Akiongea katika kikao kwenye kikao cha uzinduzi wa bodi mpya ya Chuo, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri, Sr. Shukrani Ndumilla alisema, “Tuna furaha kubwa kuona kwamba chuo cha K’s Royal kinazingatia ubora wa elimu na mafunzo yanayotolewa kwa wanafunzi wake. Hii ni hatua muhimu sana katika kuimarisha sekta ya afya na kuandaa wanachuo kuwa viongozi wa baadaye.”
Nae Mkuu wa Chuo cha K’s Royal Edward Aloyce amesema Wafanyakazi wa chuo hicho wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali, ikiwa ni pamoja na hospitali, vituo vya afya na mashirika yasiyo ya kiserikali, ili kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanazingatia mahitaji halisi ya soko. Chuo pia kina programu za mafunzo kwa vitendo, ambapo wanafunzi wanapata nafasi ya kufanya kazi katika maeneo halisi ya huduma za afya.
Amesema kuwa wanafunzi wanaofuzu kutoka chuo hicho wamekuwa wakifanya vizuri katika soko la ajira, huku wengi wakiteuliwa katika nafasi muhimu katika taasisi mbalimbali za afya. Hii ni ishara tosha ya kazi nzuri inayoendelea kufanywa na chuo hicho.
“Tutendelea kufanya kila posible kuhakikisha kuwa wanafunzi wetu wanapokea elimu bora na mafunzo yanayowafanya wawe tayari kukabiliana na changamoto za sekta ya afya. Tunashirikiana na wadau mbalimbali ili kuboresha mazingira ya kujifunza na kuwapatia wanafunzi ujuzi wanaohitaji.” – Edward
Bodi ya Ushauri imeelekeza wito kwachuo hicho kuendelea kuwa mfano ili kuimarisha ubora wa mafunzo yanayotolewa nchini, na mwisho, kuimarisha sekta ya afya kwa faida ya jamii nzima