Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

VIAZI MVIRINGO VYATAJWA KUHARIBU SOKO LA PARETO,PCT YATOA SOMO KWA MAWAKALA WA UNUNUZI NA WAKULIMA

May 9, 2025

MVUA ILIVYOATHIRI BARABARA MITAANI ITEZI MBEYA WANANCHI WAPAAZA SAUTI ,MDAU AJITOKEZA KUTOA SAPOTI

May 7, 2025

MVUA ILIVYOATHIRI MIUNDO MBINU MITAANI ITEZI MBEYA WANANCHI WAPAAZA KILIO

May 6, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • VIAZI MVIRINGO VYATAJWA KUHARIBU SOKO LA PARETO,PCT YATOA SOMO KWA MAWAKALA WA UNUNUZI NA WAKULIMA
  • MVUA ILIVYOATHIRI BARABARA MITAANI ITEZI MBEYA WANANCHI WAPAAZA SAUTI ,MDAU AJITOKEZA KUTOA SAPOTI
  • MVUA ILIVYOATHIRI MIUNDO MBINU MITAANI ITEZI MBEYA WANANCHI WAPAAZA KILIO
  • KUSUASUA KWA UJENZI BARABARA NJIA NNE JIJINI MBEYA WANANCHI WATOA MAONI YAO
  • CHAKAMWATA YAJA NA TAMKO KWA RAIS ONGEZEKO LA MSHAHARA KIMA CHA CHINI
  • MADAKTARI BINGWA 36 WA DKT SAMIA WAWEKA KAMBI SIKU 5 MBEYA KUTOA MATIBABU MIKOA NYANDA ZA JUU KUSINI
  • WAANDISHI WA HABARI KUANZA KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA TAI-HABARI – MSIGWA
  • “Meya: Deni la Kuipandisha Mbeya City Limelipwa!” Maandalizi Mapya Yaanza kwa Kishindo”
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » WATENDAJI UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA
Uncategorized

WATENDAJI UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuMay 1, 2025No Comments0 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email
Mwemyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na watendaji wa uboreshaji ngazi ya Kata na Waandishi Wasaidizi na Waendesha vifaa vya Biometriki kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa leo Aprili 29,2025 wakati alipotembelea mafunzo hayo ikiwa ni maandalizi ya awamu ya pili mzunguko wa kwanza wa uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaoanza Mei Mosi hadi Mei 07, 2025 katika mikoa 15.
Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo hayo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume.
Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo hayo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume.

 

Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akikagua
mafunzo ya watendaji wa Uboreshaji ngazi ya Kata kutoka Halmashauri ya Manispaa
ya Iringa leo Aprili 29,2025 ikiwa ni maandalizi kuelekea awamu ya pili ya
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na uwekaji wazi wa Daftari la
awali la wapiga Kura. 

 

 

 

Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akikagua
mafunzo ya watendaji wa Uboreshaji ngazi ya Kata kutoka Halmashauri ya Manispaa
ya Iringa leo Aprili 29,2025 ikiwa ni maandalizi kuelekea awamu ya pili ya
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na uwekaji wazi wa Daftari la
awali la wapiga Kura. 

 

Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Daftari na TEHAMA wa Tume.
*******
Na. Mwandishi wetu, Iringa
TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka
watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kufanya kazi kwa
kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za Uchaguzi wakati wa utekelezaji wa
awamu ya pili ya zoezi hilo litakalofanyika sambamba na uwekaji wazi wa Daftari
la Awali la Wapiga Kura ambapo mzunguko wa kwanza utahusisha mikoa 15 kuanzia
mei mosi hadi saba mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo Aprili 29,2025 na
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs
Mwambegele wakati akizungumza na washiriki wa mafunzo ya siku moja ya watendaji
hao ngazi ya Kata kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa.
“Nawakumbusha tena kama nilivyowakumbusha
katika zoezi lililopita, kwamba katika utekelezaji wa zoezi hili mzingatie sheria,
kanuni na taratibu za uchaguzi, muwe wanyenyekevu kwa wateja mtakao kuwa
mnawahudumia,”alisema Jaji Mwambegele.

Jaji Mwambegele amewaeleza watendaji hao kuwa
wateja wengi watakaowahudumia ni wananchi wa kawaida hivyo hawana budi
kuwahudumia vyema kwa lugha nzuri naikitokea kuna ulazima wa kuwarekebisha pale
wanapokosea basi wafanye hivyo kwa staha.

“Zoezi hilo linafanyika kwa mujibu wa
masharti ya kifungu cha 16(5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na
Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024 kinachoipa Tume jukumu la kuboresha Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura mara mbili mara baada ya uchaguzi mkuu na kabla ya uteuzi
wa wagombea kwa uchaguzi mkuu unaofuata,” alisema.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura awamu ya pili utafanyika sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la
Wapiga Kura kuanzia tarehe 01 Mei, 2025 na kukamilika tarehe 04 Julai, 2025.

Uboreshaji wa Daftari unataraji kufanyika kwa
mizunguko mitatu ambapo mzunguko wa kwanza utajumuisha mikoa 15, mzunguko wa
pili mikao 16 na mzunguko wa tatu utajumuisha vituo vya magereza na vyuo vya
mafunzo.

Mikoa itakayohusika kwenye mzunguko wa kwanza
wa uboreshaji ni pamoja na Iringa, Geita, Kagera, Mara, Shinyanga, Mwanza,
Simiyu, Rukwa, Tabora, Katavi, Kigoma, Ruvuma, Mbeya, Njombe na Songwe ambapo
zoezi hilo litafanyika kuanzia Mei 1 hadi 7 mwaka huu.

Aidha, mzunguko wa pili utahusisha mikoa ya
Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Dar es
Salaam, Lindi, Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini
Pemba na Kusini Pemba ambapo zoezi hilo litafanyika kuanzia Mei 16 hadi 22,
2025.

Mzunguko wa tatu wa zoezi la uboreshaji wa
Daftari utahusisha vituo 130 vilivyopo kwenye magereza ya Tanzania Bara na
vituo 10 vilivyopo katika Vyuo vya Mafunzo Tanzania Zanzibar kwa wakati mmoja
na utafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia Juni 28 hadi Julai 04, 2025.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura kwa awamu ya pili, utafanyika ngazi ya kata kwa Tanzania Bara na ngazi ya
jimbo kwa Tanzania Zanzibar, ambapo jumla ya vituo 7,869 vitahusika, vituo
7,659 vipo Tanzania Bara na vituo 210 vipo Tanzania Zanzibar.

Katika awamu ya pili ya uboreshaji, wapiga
kura wapya 1,396,609 wataandikishwa, wapiga kura 1,092,383 wataboresha taarifa
zao na wapiga kura 148,624 watafutwa kwenye Daftari kwa kukosa sifa za
kuendelea kuwepo kwenye Daftari,” amesema Jaji Mwambegele.

Mambo mengine ni kuhamisha taarifa za wapiga
kura waliohama kutoka kata au jimbo walipoandikishwa awali na kuondoa  taarifa za wapiga kura waliopoteza sifa za
kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.

Aidha, kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha
11(1) na (2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka
2024, Tume pia ina jukumu la kuandaa Daftari la Awali la Wapiga Kura na
kuliweka wazi kwa umma.

Lengo la uwekaji wazi wa Daftari hilo ni
kutoa fursa kwa wananchi kukagua, kufanya marekebisho ya taarifa za wapiga kura
na uwekaji wa pingamizi dhidi ya wapiga kura waliomo kwenye daftari ambao
hawana sifa na litabandikwa katika vituo vyote vilivyotumika wakati wa
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza.

Tume iliboresha Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura awamu ya kwanza kuanzia tarehe 20 Julai, 2024 na kukamilisha tarehe 25
Machi, 2025.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

SERIKALI ITAFANYIA KAZI HARAKA MAAZIMIO YA KONGAMANO LA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI- MSIGWA.

April 29, 2025

Tiba ya uhakika ya ugonjwa kisukari

January 24, 2025

Mpenzi wangu alinitapeli Sh5.7 milioni ila amezirudisha mwenyewe!

January 8, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024169

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202481

DKT. TULIA ATOA MSAADA WA VIPAZA SAUTI MSIKITI WA MASJID BI FATMA NZOVWE JIJINI MBEYA

March 29, 202457

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI MBEYA YAANZA,WANAHABARI WATEMBELEA MIRADI

March 16, 202444
Don't Miss
Video Mpya

VIAZI MVIRINGO VYATAJWA KUHARIBU SOKO LA PARETO,PCT YATOA SOMO KWA MAWAKALA WA UNUNUZI NA WAKULIMA

By Mbeya YetuMay 9, 20250

#mbeyayetutv

MVUA ILIVYOATHIRI BARABARA MITAANI ITEZI MBEYA WANANCHI WAPAAZA SAUTI ,MDAU AJITOKEZA KUTOA SAPOTI

May 7, 2025

MVUA ILIVYOATHIRI MIUNDO MBINU MITAANI ITEZI MBEYA WANANCHI WAPAAZA KILIO

May 6, 2025

KUSUASUA KWA UJENZI BARABARA NJIA NNE JIJINI MBEYA WANANCHI WATOA MAONI YAO

May 5, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

VIAZI MVIRINGO VYATAJWA KUHARIBU SOKO LA PARETO,PCT YATOA SOMO KWA MAWAKALA WA UNUNUZI NA WAKULIMA

May 9, 2025

MVUA ILIVYOATHIRI BARABARA MITAANI ITEZI MBEYA WANANCHI WAPAAZA SAUTI ,MDAU AJITOKEZA KUTOA SAPOTI

May 7, 2025

MVUA ILIVYOATHIRI MIUNDO MBINU MITAANI ITEZI MBEYA WANANCHI WAPAAZA KILIO

May 6, 2025
Most Popular

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024169

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202481

DKT. TULIA ATOA MSAADA WA VIPAZA SAUTI MSIKITI WA MASJID BI FATMA NZOVWE JIJINI MBEYA

March 29, 202457
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.