Mafunzo kwa Shirikisho la askari wa kike na wasimamizi wa sheria duniani yameendelea katika Jiji la
Chicago Nchini Marekani ambapo mada na masomo mbalimbali yameendelea ambapo suala la
wahamiaji na changamoto zake kutokana na mabadiliko ya Sheria baina ya Nchi na Nchi likamulikwa na
washiriki wakapata nafasi ya kubadilisha uzoefu namna ya kukamiliana na changamoto hizo.
Akiongea mara baada ya mafunzo hayo Naibu kamishna wa uhamiaji DCI Tatu Burhan amesema kuwa
masomo waliojifunza yalijikita katika masuala ya ushirikiano wa kimataifa na utatuzi wa changamoto za
wahamiaji wanaoingia katika mataifa mbalimbali na namna bora ya kuzitatu changamoto hizo.
Ameongeza kuwa masomo hayo waliofundishwa yamewapa namna bora ya kukabiliana changamoto za
wahamiaji ambao wamekuwa wakiingia katika nchi tofauti tofauti kwa lengo la makazi akaweka wazi
kuwa suala la wahamiaji ni suala mtambuka linalotegemea sera zitakazoleta mabadiliko ya kukabiliana
na changamoto za wahamiaji wanaoingia katika mataifa husika.
Aidha DCI Tatu akabainisha kuwa mafunzo waliyoyapata pia yamewakumbusha suala la matumizi ya
teknolojia ili kukabiliana na wahamiaji ambao wanaingia katika nchini bila ya kufuata taratibu ambapo
alisema kuwa zipo sababu zinazomfanya mtu kuingia katika nchi husika, huku akitumia fursa hiyo kutoa
wito kwa watanzania kuendelea kushirikiana na idara hiyo katika kutoa taarifa za wahamiaji haramu ili
kukabiliana na changamoto hiyo.
Nae Mkufunzi Kutoka Wizara ya huduma za Binadamu Chicago ambaye aliyetoa mada na mafunzo ya
masuala ya mipaka na wahamiaji Bwana Ronald Vitiello akaeleza namna alivyoweza kubadilisha uzoefu
na washiriki wa mafunzo hayo katika jiji la Chicago ambapo amesema mafunzo hayo yalikuwa ni juu ya
changamoto za mipaka katika maeneo ya Marekani na Mexico na mipaka kwa ujumla.
Ronald akaweka wazi kuwa wamejadiliana na kubadilisha uzoefu akieleza mgogoro baina ya Marekani
na Mexico na athari zake kwa uhusiano na ushirikiano wa kimataifa Pamoja na sheria za upelelezi.
Mafunzo hayo yanaendelea huku mada mbalimbali zikifundishwa ili kuwajengea uwezo wa kiutendaji
washriki wa mafunzo hayo hayo ambayo kidunia yanafanyika Chicago Nchini Marekani yakihisha Mataifa
zaidi ya siti na Nne.
Na. Abel Paul Chicago Marekani.