Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Solomon Itunda amekutana na kufanya mazungumzo ya namna ya Shirika hilo litakavyoendelea kutoa huduma ya matibabu ya macho kwa wananchi wa wilaya hiyo.Mhe. Itunda amekutana na viongozi hao leo Ijumaa Novemba 15, 2024 kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya iliyopo Mkwajuni.Katika mazungumzo yao, Mhe. Itunda amewashukuru viongozi hao kwa kutoa huduma ya msaada wa utatuzi wa changamoto ya macho kwa wananchi kupitia mpango wao wa miaka miwili.
“Leo nimekutana na wawakilishi wa Shirika la Helen Keller International lililoanzishwa nchini mwaka 1984 na lenye Makao yake Makuu jijini Daresalam linalojihusisha na utoaji wa huduma ya matibabu ya macho” amesema DC Itunda na kuongeza;
“Katika Wiliya ya Songwe kupitia mpango wao wa miaka miwili, waliweza kutoa huduma kwa wananchi 600 ambao walikuwa na changamoto mbali mbali za magonjwa ya macho. Nawashukuru sana kwa mchango wao”
Wajumbe wa shirika hilo waliongozwa na waratibu ndugu Ibrahim Babu na ndugu Antidius Banulirwa.