Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Meneja Mahusiano Idara ya Wateja Binafsi – Luiana Keenja, alipotembelea Banda la NMB kwenye Maadhimisho ya wiki ya Vijana katika viwanja vya Soko la Uhindini jijini Mbeya katikati ni Meneja Mauzo Kanda Nyanda za Juu Ungandeka Mwakatage.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete ameipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kuwa karibu na Wananchi kwa kusogeza huduma kwa watu wa maeneo ya pembezoni.
Kikwete ameongea hayo alipotembelea Banda la NMB kwenye Maadhimisho ya wiki ya Vijana viwanja vya Soko la Uhindini jijini Mbeya.
Amesema Benki hiyo ambayo kwa asilimia kubwa inawahudumia watumishi wa umma imewafikia wateja wengi wa pembezoni na hivyo kuwavutia wateja wengi kufungua akaunti katika benki hiyo.
Akizungumza wakati akimkaribisha Waziri Kikwete, Meneja Mahusiano Mwandamizi wa Benki ya NMB Josephine Kulwa amesema kwa kuzingatia umuhimu wa Wiki ya Vijana nchini Benki ya NMB imeshiriki kikamilifu maadhimisho hayo sanjari na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambapo Benki hiyo imekuwa mmoja wa Wadhamini wakuu.
Kulwa amesema Huduma za kibenki za NMB zimelenga pia makundi ya vijana,ikiwemo akaunti maalumu ya Mwanachuo Account, Chimbo la Chuo (GO na NMB) ambapo Mwanachuo akifanya muamala kwa Lipa Namba ya NMB hurudishiwa hadi asilimia 30 na mafunzo kwa vitendo.
Na Mwandishi Wetu Mbeya