Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI

February 15, 2026

SHEIKH WA MKOA MBEYA ATOA UJUMBE KWA WAISLAMU KUELEKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

February 15, 2026

EFTA YACHOCHEA UCHUMI KWA HATI FUNGANI YA BILIONI 50

February 14, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI
  • SHEIKH WA MKOA MBEYA ATOA UJUMBE KWA WAISLAMU KUELEKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN
  • EFTA YACHOCHEA UCHUMI KWA HATI FUNGANI YA BILIONI 50
  • Kanisa la Moravian Tanzania Lamkabidhi Yona Sonelo Tuzo Maalum Baada ya Shahada ya Heshima Australia
  • Beno Malisa Azindua Tawi la Strategies Insurance Mbeya, Akaribisha Wawekezaji
  • RC Malisa Afungua Mafunzo ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi Mbeya
  • CRDB YAUNGANA NA JESHI LA POLISI MBEYA KUELEKEA SIKU MAALUM YA POLISI.
  • DAS Mbeya: Kipato Kisiharibu Vyanzo vya Maji
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI
Habari za Kitaifa

AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI

Mbeya YetuBy Mbeya YetuFebruary 15, 2026Updated:February 15, 2026No Comments3 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imebainisha haja ya kufanya mapitio ya haraka ya Sera na Sheria ya Huduma za Habari nchini ili kuendana na kasi kubwa ya mabadiliko ya teknolojia ya kidijitali.
Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa sheria hiyo, iliyotungwa mwaka 2016 kabla ya ukuaji wa sasa wa mitandao ya kijamii, inatoa tafsiri pana itakayowawezesha bloga na watengeneza maudhui ya mtandaoni kutambulika na kusimamiwa kisheria.

Kutokana na mazingira ya sasa, JAB inaona kuna umuhimu wa kufanya mapitio hayo ili kuyaingiza katika mfumo makundi hayo mapya yanayochipukia kwa kasi katika tasnia ya habari.
Katika wasilisho lililotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula, katika mkutano wa mwaka wa utangazaji 2026 jijini Dodoma, imeelezwa kuwa mfumo rasmi wa ithibati umewekwa kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229, kwa lengo la kulinda maslahi ya umma na kuimarisha maadili ya kitaaluma.

Kwa sasa, JAB inasimamia utambuzi wa wataalamu wa habari kupitia mfumo wa kidigitali wa TAI-HABARI, ambapo waandishi waliokidhi vigezo hupatiwa vitambulisho (Press Cards) vyenye uhalali wa miaka miwili. Hadi kufikia Januari 2026, takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya maombi 3,200 yameidhinishwa, huku maombi mengine yakiendelea kufanyiwa kazi.

Licha ya mafanikio hayo, Bodi imetaja kuwepo kwa changamoto ya mtazamo hasi miongoni mwa baadhi ya wadau ambao wanaiona ithibati kama chombo cha kudhibiti badala ya nyenzo ya kuimarisha ubora wa uandishi.

Aidha, uelewa mdogo wa sheria umekuwa ukisababisha baadhi ya waandishi kuwasilisha maombi yasiyokidhi vigezo vya kitaaluma, ikiwemo hitaji la kuwa na angalau Stashahada au Shahada ya Uandishi wa Habari. JAB imesisitiza kuwa mwandishi asiye na ithibati hukosa uhalali wa kisheria na anaweza kuchukuliwa hatua kali, huku ikionya kuwa hali hiyo inadhoofisha uaminifu wa habari nchini.

Wakili Kipangula amesema kwamba Bodi imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari kwa kushirikiana na mamlaka nyingine kama TCRA na taasisi za elimu ili kuhakikisha kuwa ithibati inatumika kama nyenzo ya kumlinda mwandishi katika utekelezaji wa majukumu yake, kumpatia ulinzi wa kitaaluma dhidi ya vitisho, na kuhakikisha jamii inapata habari sahihi na za kweli.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

EFTA YACHOCHEA UCHUMI KWA HATI FUNGANI YA BILIONI 50

February 14, 2026

KUMBUKUMBU YA EDWARD NGOYAI LOWASSA

February 10, 2026

JK KWA MFALME MSWATI III KUJADILI UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA KWA NCHI WANACHAMA WA ECSA

February 4, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025344

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024230

Vijana Wamchana Waziri wa Vijana, ”Si Wananchi, Ila Watumishi Ndio Watakaoniangusha”

December 1, 2025140
Don't Miss
Habari za Kitaifa

AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI

By Mbeya YetuFebruary 15, 20263

Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imebainisha haja ya kufanya mapitio ya haraka…

SHEIKH WA MKOA MBEYA ATOA UJUMBE KWA WAISLAMU KUELEKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

February 15, 2026

EFTA YACHOCHEA UCHUMI KWA HATI FUNGANI YA BILIONI 50

February 14, 2026

Kanisa la Moravian Tanzania Lamkabidhi Yona Sonelo Tuzo Maalum Baada ya Shahada ya Heshima Australia

February 14, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI

February 15, 2026

SHEIKH WA MKOA MBEYA ATOA UJUMBE KWA WAISLAMU KUELEKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

February 15, 2026

EFTA YACHOCHEA UCHUMI KWA HATI FUNGANI YA BILIONI 50

February 14, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025344

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024230
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.