Author: Mbeya Yetu

Kijungu na Daraja la Mungu ni maeneo maarufu ya kijiografia na vivutio vya utalii nchini Tanzania, vilivyopo katika mkoa wa Mbeya, Nyanda za Juu Kusini. Zina sifa za asili za kijiolojia zinazovutia watalii na watafiti wa mazingira.

Kijungu
Kijungu ni eneo la kijiolojia lenye sura ya mto unaozunguka mwamba mkubwa, na kuacha mduara kama “jungu” (sufuria), na ndilo linalotoa jina lake. Hapa maji ya mto huchonga mwamba kwa nguvu, na kuacha mandhari ya kuvutia. Kijungu kinajulikana kwa nguvu zake za maji ya maporomoko ambayo yamepita hapo kwa miaka mingi, na kuunda maumbo haya ya kustaajabisha.

Daraja la Mungu
Daraja la Mungu ni jiwe kubwa lililojitengeneza kiasili na kuonekana kama daraja la asili. Inasemekana kuwa ni sehemu ya maporomoko ya maji ambayo maji yamechonga miamba kwa muda mrefu, na kuacha mwamba huo mkubwa ukionekana kama daraja. Jina “Daraja la Mungu” limetokana na imani za wenyeji kuwa daraja hilo limeundwa kwa nguvu za kimuujiza, kutokana na umbo lake la kipekee.

Maeneo haya yote ni sehemu muhimu za utalii wa mazingira nchini Tanzania, na huvutia watu wanaopenda urembo wa asili, kijiolojia, na historia ya asili ya Tanzania.

Read More

Samadi ya ng’ombe imekuwa ikuchukuliwa kama uchafu unaochangia uharibifu wa mazingira mitaani, lakini kwa wananchi wa Wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwao hali ni tofauti kwani sasa wanaityumia samadi hiyo kuokoa uhribifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa. Makala haya yanaelezea namna wananchi hao wanavyotumia samadi hiyo kutengeneza gesi ya kupikia (Biogas),.

Read More

Tabia ya baadhi ya Wazazi kuwapiga watoto wao kupita kiasi bila kujali athari za kiafya na kisaikolojia zitakazompata mtoto husika ni aina ya ukatili kwa watoto.. Makala hii inaeleza madhara yaliyompoata mtoto mmoja wa kike wilyani Mbozi mkoani Songwe baada ya kupigwa na Baba yake mzazi kwa tuhuma za kuiba pesa nyumbabni.kwao. Kupitia mradi wa Ulinzi na Usalama wa mtoto Shirika la Intergrated Rule Development Organisation limeingilia kati ukatili huoili kumuokoa mtoto huyo dhidi ya ukatili aliofanyiwa.

Read More

Na. Mwandishi Jeshi la Polisi Arusha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limezindua kampeni ya tuwaambie kabla hawajaharibiwa kwa lengo la kuongea na wanafunzi kuanzia elimu ya awali hadi vyuo vikuu kwa ajili ya kuwaelimisha juu ya kujitambua ili kujiepusha na vitendo vya mmomonyoko wa maadili.

Akizungumza katika uzinduzi huo ambao umehudhuriwa na washiriki zaidi ya 3,000, Katibu Tawala Msaidizi viwanda Biashara na uwekezaji Mkoa wa Arusha Bw. Frank Mbando ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amewataka wanafunzi kuhakikisha wanajitunza vyema na kuwa makini na rika walilopo kwa kujiepusha na vitendo ambavyo vitaharibu maisha yao ya sasa na ya baadaye.

Aidha amebainisha kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika elimu kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bure yenye ubora ambapo amesema hadi sasa zaidi ya shilingi bilioni saba zimeshatolewa tangu serikali ya awamu ya sita iingie madarakani.

Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi SP Happiness Temu amesema lengo la kampeni hiyo ni kuwatahadharisha wanafunzi wa shule za awali Msingi, Sekondari na vyuo vya juu kuacha kuiga tabia mbovu ambazo hazina tija katika ustawi wa Maisha yao ya kila siku na masomo.

SP Temu amebainisha kuwa kupitia elimu ambayo itaenda kutolewa itasaidia kujenga taifa litakalokuwa na kizazi chenye maadili mema na raia wema wanaojitambua kabla ya kupitia mapito ya ukatili.

Kamanda wa Kikosi Cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua amesema dhima ya Jeshi la Polisi kupitia kampeni hiyo ni kuhakikisha linayafikia makundi yote ya wanafunzi kuanzia shule za awali, msingi, sekondari na vyuo vya ngazi zote kuzungumza nao kuwapa elimu ya kujitambua mapema.

Katika uzinduzi wa Kampeni hiyo Washiriki zaidi ya 3,000 ambao ni Jeshi la Polisi, Shule zaidi ya 10, vyuo 12 pamoja na Wananchi walishiriki.

Read More

Watumishi wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Dodoma wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na upendo ili kuweza kutekeleza mpango kazi wa Taasisi. Hayo yamesema na Meneja wa TARURA mkoa wa Dodoma, Mhandisi Edward Lomelo wakati wa mafunzo ya VVU/UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza yaliyofanyika Eneo la Michoro ya Miambani Kolo wilayani Kondoa. “Tunafanya kazi kubwa za kuboresha barabara na tunapokea mrejesho mzuri toka kwa wananchi hivyo nawataka watumishi wote tufanye kazi kwa ushirikiano na upendo”. Kuhusiana na mada walizofundishwa na wataalam wa afya alisema watumishi kama wazazi wanapaswa kuwalinda watoto wa kiume na wa kike…

Read More

Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imekamilisha ujenzi wa daraja la Msadya lenye urefu wa mita 60 na upana mita 10.5 pamoja na ujenzi wa barabara unganishi ya Kibaoni-Chamalendi-Mdede kwa gharama ya shilingi bilioni 4.2 katika Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi.Meneja wa TARURA Wilaya ya Mlele, Mhandisi Paul Mabaya, ameishukuru serikali kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Msadya lenye uwezo wa kupitisha magari tani 30 ambalo limenufaisha wananchi wa kata za Mwamapuli, Chamalendi, Ikuba, Kibaoni na Majimoto kusafirisha mazao yao.“Daraja hili limekuwa mkombozi, shughuli kubwa hapa ni kilimo na ufugaji, kiasi…

Read More