Author: Mbeya Yetu

Afisa anayeshughulikia malamiko Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA)Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Francis Mhina amesema taasisi yake imerahisisha upatikanaji wa ujenzi wa vituo vya mafuta maeneo ya mijini na vijijini.

Ameyasema hayo katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Nyanda za Juu yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale Jijini Mbeya.

Katika hatua nyingine Mhina amesema mwananchi mwenye malalamiko juu ya utendaji usioridhisha kutoka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira,Shirika la Umeme na Vituo vya mafuta ofisi yake ipo wazi kupokea chamoto hizo.
Tobieta Makafu Afisa Uhusiano Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA)Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambayo inahudumia Mikoa ya Mbeya,Njombe,Songwe na Rukwa amesema endapo mwananchi atauziwa mafuta kinyume na bei elekezi asisite kutoa taarifa EWURA.

Read More

Wananchi Mikoa ya Nyanda za Juu wamejitokeza kwa wingi kutembelea Uwanja wa Maonesho John Mwakamgale hususani katika banda la Baraza la Taifa la usimamizi wa Mazingira(NEMC).

Tilika Mwambungu ni Afisa Mazingira Kanda ya Nyanda za Juu Kusini anaeleza elimu wanayoitoa katika banda lao.

Baadhi ya washiriki waliotembelea banda hilo wamefurahishwa na huduma zinazotolewa wakiwemo wanafunzi wa shule ya msingi Scripture Union iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya.

Baraza la Taifa la usimamizi wa Mazingira(NEMC) limetilia mkazo kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira na hutumia maonesho mbalimbali kufikisha ujumbe kwa jamii.

Read More

Kazi ya kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wanaotembelea banda la Mama Samia Legal Aid Campaign, ikiendelea kwenye maonesho ya nanenane jijini Dodoma Na Mwandishi Wetu BAADA ya kusaidia maelefu ya Watanzania kupitia maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF), Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia au maarufu kama Mama Samia Legal Aid Campaign, sasa iko katika maonesho ya nanenane jijini Dodoma. Kampeni hiyo ambayo tangu kuzinduliwa kwake mwaka jana, imekuwa ikitumia wabobezi katika tasnia hiyo ya sheria kutatua migogoro mbalimbali inayotokea kwenye jamii katika mikoa mbalimbali wanakopita iko katika maonesho hayo…

Read More