Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- POLISI NA WANAHABARI MBEYA WAWEKA MIPANGO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
- Yamenifika makubwa baada ya kuikataa mimba yake
- Happy birthday Dr. Tulia
- Viongozi 11 wa CHADEMA washikiliwa na Polisi Mkoa wa Songwe
- ZIARA YA NAIBU WAZIRI MAHUNDI ZANZIBAR
- Jinsi ya Kufikisha Malalamiko Kuhusu Mradi wa REGROW na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
- Naibu Waziri Mhandisi Maryprisca Mahundi Akagua Hali ya Mawasiliano Kisiwani Kojani, Pemba
- Inauma sana: Mtoto wangu kaenda chuo kikukuu katumbukia katika umalaya na dawa za kulevya
Author: Mbeya Yetu
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera ameagiza kukamatwa na kichunguzwa viongozi wa chama kikuu cha ushirika wilayani Kyela (KYECU) Kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kupelekea upotevu wa zaidi ya millioni 440 za wakulima, baada ya magunia zaidi ya 200 kutoonekana baada ya mnada namba tatu wa zao la cocoa uliofanyika jumatatu July 15 wilayani humo.
Pamoja na kukamatwa viongozi hao akiwemo mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wilayani Kyela (KYECU) Evance Mwaipopo pamoja na Meneja wa chama hicho Julius Mwankenja, Homera ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Mbeya, kuchunguza chama hicho mifumo yao ya kifedha huku akisitisha taratibu zote za manunuzi Hadi pale kamati ya ulinzi na usalama itakapo jiridhiaha.
Awali akiwasilisha taarifa Kwa mkuu wa Mkoa, mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe Josephine Manasi, amesema hasara hiyo imeonekana baada ya mnunuzi aliyeshinda mnada namba tatu kubaini magunia zaidi ya 200 hayopo kwenye maghara kati ya magunia 1,915 yaliyoshindanishwa kwenye mnada huo.
Baadhi ya wanawake wanafunzi a wananchi wakiwa kwenye Banda la DMI katika Maonesho yaTano ya Elimu Juu Zanzibar. Makamu Mkuu wa Chuo cha DMI (Taaluma) Dkt.Wilfred Johnson Kileo akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Maonesho ya ya Tano Wiki ya Elimu ya Juu inayofanyika Viwanja vya Maisara Zanzibar DMI yawaasa Wasichana kujiunga kada ya Ubahari *Yasema hakuna kizuizi cha kufanya mwanamke kuwa baharia Na Mwandishi Wetu,Zanzibar Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimewataka wahitimu wanawake wa kidato cha sita cha mwaka huu kujitokeza kujiunga na kada ya ubaharia katika chuo hicho. Kauli hiyo ameitoa jana Makamu Mkuu…
Kituo cha Radio Highlands Fm 92.5 Mbeya kwa kushirikiana na Kampuni ya 3 Ocean imezindua mchezo wa kubahatisha nchini unaofahamika kwa jina la Vuna Deile ambapo Washindi watajinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo gari,pikipiki,TV na pesa taslimu. Akitoa taarifa kwa Wanahabari Mkurugenzi wa Kituo cha Radio Highlands Fm Mbeya Jacqueline Mwakyambiki amesema mchezo huu wa Vuna Deile ni rahisi utachezwa na mtu yeyote kwa njia ya simu yake ya mkononi ambako Radio inasikika nchini na unachezwa kuanzia kiasi cha shilingi mia mbili tu. Jacqueline amewataka wananchi kuichangamkia fursa hii hususani wale wa Mikoa ya Mbeya,Songwe na Njombe kwani ni wa kusisimua ambao…
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYAUWSA)CPA Kayange amesema Mamlaka yake imetenga siku mbili katika juma kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali. CPA Kayange amesema mradi wa Hasara na Hanza utahudumia Kata ya Iganzo,Ilemi na Mwasenkwa ambapo wananchi wameaswa kuchangamkia fursa hiyo na kwamba wananchi wanaweza kulipa kidogo kidogo kwa makubaliano maalum. Kayange amesema mradi umefikia asilimia themanini ambapo mpaka sasa zaidi ya kaya mia moja thelathini zimenufaika na mradi huo. Hata hivyo amesema maboresho yanayofanywa katika chanzo cha Nzovwe utakaonufaisha wananchi wa Isyesye. Aidha amesema mradi wa maji mto Kiwira umefikia asilimia thelathini. Kayange…
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi chuo cha VETA cha Mkoa wa Rukwa kilichopo katika kijiji cha Kashai, Kata ya Momoka, wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, leo tarehe 16 Julai, 2024, ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Rukwa. Akizungumza na wananchi waliohudhuria hafla hiyo mara baada ya kuweka jiwe la msingi, Mhe. Rais amesema kwa sasa mkoa wa Rukwa unakua kiuchumi, hasa katika eneo la miradi mbalimbali ya maendeleo, hivyo ni wakati wa vijana na jamii kwa ujumla kupata chuo cha kuwawezesha kupata ujuzi, utaalamu na maarifa ili waweze kuendana…
Matukio mbalimbali katika picha Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi aalipotembelea makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo Julai 16, 2024 jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akioneshwa namna Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ikifanya ufuatiliaji wa maudhui ya watoa huduma wa sekta ya utangazaji alipotembelea makao makuu ya Mamlaka hiyo leo Julai 16, 2024 jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akimsikiliza Dkt. Jabiri Kuwe, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania akimfafanulia…