Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- POLISI NA WANAHABARI MBEYA WAWEKA MIPANGO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
- Yamenifika makubwa baada ya kuikataa mimba yake
- Happy birthday Dr. Tulia
- Viongozi 11 wa CHADEMA washikiliwa na Polisi Mkoa wa Songwe
- ZIARA YA NAIBU WAZIRI MAHUNDI ZANZIBAR
- Jinsi ya Kufikisha Malalamiko Kuhusu Mradi wa REGROW na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
- Naibu Waziri Mhandisi Maryprisca Mahundi Akagua Hali ya Mawasiliano Kisiwani Kojani, Pemba
- Inauma sana: Mtoto wangu kaenda chuo kikukuu katumbukia katika umalaya na dawa za kulevya
Author: Mbeya Yetu
UMWAGAJI ZEGE UJENZI WA BANIO MRADI MTO KIWIRA WAANZA
Miradi wa Maji mto Kiwira unaendelea kwa ufanisi mkubwa kama ilivyokusudiwa na kasi ikielekezwa kwenye umwagaji wa zege kwenye banio utakaodumu kwa saa thelathini na sita unaofanywa na kampuni ya China Railway Construction Group ambapo awali ilifanyika kazi ya kuchepusha mto.
Hayo yamebainishwa na Mhandisi Barnabas Konga Mkurugenzi wa masuala ya Ufundi Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYAUWSA) ambaye pia ni Msimamizi wa mradi wa Maji mto Kiwira.
Konga amesema shughuli ya zege itafanyika usiku na mchana ili ifikapo mwezi machi mwakani mradi uwe umekamilika.
Aidha Konga amempongeza Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson kwa ufuatiliaji wa pesa za mradi sanjari na kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa za utekelezaji wa mradi.
Konga amesema vijiji vya Unyamwanga, Mbeya 1 na Swaya vinavyopitiwa na mradi huo vitanufaika na huduma ya maji.
Robert Mkasela kutoka kampuni ya GKW anayemsimamia mkandarasi amesema mradi unasimamiwa kwa ubora, usalama na wakati uliokusudiwa.
Kwa upande wake Wang Yang mkandarasi wa mradi huo amesema mradi utakamilika kama ilivyokusudiwa lengo ni kukamilisha banio na tanki la kupokelea maji kabla ya msimu wa mvua kuanza.
Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Julai 8,2024 mkoani Tabarea. Washiriki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo. Washiriki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo. Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza kwa wadau wa Mkoa wa Tabora. Mkurugenzi wa Idara ya Daftari na TEHAMA wa Tume, Stanslaus Mwita akiwasilisha mada ya mfumo. …
Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazo nufaika na mradi wa Sustainable Ocean Phase II”unaosimamiwa na Taasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu nchini Denmark(Danish Institute of Human Rights). Hayo yamebainishwa na Mshauri Mkuu wa Taasisi hiyo Bi.Carol Rask wakati walipotembelea Ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora hivi karibuni Jijini Dodoma. Bi.Carol alisema mradi huo unaotarajiwa kutaekelezwa kwa muda wa miaka minne unafadhiliwa na SIDA. mradi huo umelenga kuimarisha ulinzi wa mazingira kwa wavuvi wadogo na jamii zinazowazungukaalisema Bi.Carol Aidha Bi Carol alisema katika kutekeleza mradi huo wamefanya ziara nchini Tanzania iliyolenga kutafuta wadau mbalimbali ambapo moja…
Bilioni 5.3 kujenga soko la Kimataifa la ndizi Kiwira Rungwe
Jumla ya shilingi bilioni 5.3 kujenga soko la Kimataifa la ndizi eneo la Kalasha Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Rungwe Gabriel Mwakagenda katika mkutano Maalumu na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Kata ya Katumba.
Mwakagenda amesema kuanzishwa kwa soko hilo mbali ya kuongeza kipato kwa Halmashauri kutanufaisha pia wakulima wa ndizi ambao watanufaika na bei nzuri kwa wanunuzi kutoka nje ya nchi.
Baadhi ya wakulima wa zao la ndizi wameomba kuharakishwa kwa mchakato wa ujenzi ili bidhaa zao zipate bei nzuri sanjari na kuwaondolea kadhia ya kuuzia ndizi kwenye tope.
Wananchi kijiji cha Ichesa Mbozi Mkoani Songwe wachangia maji ya kunywa pamoja na mifugo, katika maisha yao hawajawahi kufungua bomba za maji safi na salama ya kunywa Diwani wa kata ya Mahenje Japhet Ntandala ahaha kutafuta ufumbuzi wa tatizo