Author: Mbeya Yetu

Mgogoro wa uwanja wa Kanisa la Gofan na Jiji umechukua sura mpya baada ya Kanisa hilo kugoma kwenda mahakamani kama walivyoshauriwa na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson Kanisa likidai mgogoro ulikwisha.
Kikao cha mwisho kilichofanyika hivi karibuni ambacho kilihudhuriwa na Dkt Tulia Ackson na kuzisikiliza pande zote ambapo alilishauri Kanisa kwenda mahakamani ili Kanisa liweze kupata haki yake.
Siku chache baada ya ushauri huo Mchungaji John Ikowelo na waumini wake wamejitokeza kufanya usafi eneo linalogombaniwa ambapo Mchungaji amesema yeye hawezi kuishitaki serikali kwani serikali imemfanyia mambo mengi na ilimaliza kabisa mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi.

Nao baadhi ya waumini wamesema mgogoro umekwisha wanachosubiria ni kibali cha ujenzi ambacho Jiji wanasita kuwapatia kwa muda mrefu hivyo wameamua kufanya usafi kwenye uwanja wao ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa Kanisa.

Mgogoro umedumu kwa zaidi ya miaka kumi ambapo kila upande unadai hilo ni eneo lake Jiji wakidai ni la shule ni eneo oevu halipaswi kujengwa nyumba huku Kanisa likidai eneo ni halali yao.

Read More

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tulia Trust Mhe. Dkt. Tulia Ackson amekabidhi nyumba Kwa Singwava Jackson mkazi wa mtaa wa ltanji Kata ya Iganjo Jijini Mbeya mjane mwenye watoto sita baada ya kuishi kwenye nyumba ya maturubai Kwa zaidi ya miaka minne. Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi,Seikali,Viongozi wa Dini,viongozi wa Mila na wananchi ambapo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera.Katika hotuba yake Dkt Tulia amewashukuru…

Read More

#mbeyayetutv
SWALA YA EID EL FITRI MBEYA.

WAUMINI wa dini ya Kiislamu Jijini Mbeya wameungana na waumini wengine kote duniani kwa kuswali Swala ya Eid El Fitri huku wakikumbushwa kuyaenzi na kuendelea kuyatekelezaa mafundisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Ibada ya Swala ya Eid imefanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa kumbukumbu ya Sokoine ukihudhuriwa na viongozi wa serikali,ujumbe ukitolewa na Spika wa Bunge la Jamuhuri Dkt, Tulia Ackson, Mkuu wa mkoa Mbeya Juma Homera na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge.

Read More

Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust ametoa futari kwa wakazi wa Jiji la Mbeya.Katika hafla hiyo Dkt Tulia Ackson amewakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera ambaye amesema Dkt Tulia amefanya mengi kwa Jiji la Mbeya ikiwemo vifaa vya ujenzi kwa shule mbalimbali sanjari na kutoa bima za afya kwa wazee zaidi ya elfu sita.Shekhe wa Mkoa wa Mbeya Msafiri Ayasi Njalambaha amesema Dkt Tulia Ackson amekuwa akisaidia jamii bila kujali itikadi zao kama kuwasaidia vifaa vya…

Read More

Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wakitorosha mifugo 514 Kwenda Nchi Jirani huku wakitumia vibali vya kampuni isiyohusika na Mifugo hiyo.Akitoa taarifa hiyo kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo Nchini kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua amesema Kikosi hicho kwa kushirikina na wananchi Aprili 06,2024 Katika Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha waliwakama watu wawili wakiwa na mifugo 514 ambayo walikuwa wakiitorosha Kwenda nchi Jirani.Kamanda Pasua amebainsha kuwa watuhumiwa hao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi huku akiwaomba wananchi kutoa taarifa za watu…

Read More

#Mafanikio ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia#

■Wizara imefanya jitihada kubwa za kukuza utalii kusini kupitia mradi wa REGROW.
■REGROW imesaidia uboreshaji na ujenzi wa viwanja vya ndege katika maeneo ya hifadhi za Taifa Mikumi, Ruaha, Udzungwa, na Nyerere.
■ Ujenzi wa majengo ya utalii na watumishi katika Hifadhi za Taifa Ruaha,Udzungwa, Mikumi na Nyerere.
■Jumla ya Vijiji 61 vinavyozunguka Hifadhi vimenufaika kwa kuwezeshwa kujiendesha kupitia vikundi vya COCOBA takribani 762.
■Miradi takribani 150 iliyoibuliwa na vikundi imetekelezwa.

Read More

Naibu Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka Maafisa Habari nchini kuwa wabunifu,weledi na kufanya kazi kwa uweledi ili kukuza tasnia ya Habari sanjari na kuisaidia serikali katika utendaji wake.Ameyasema hayo April 5,2024 ukumbi wa St Peters Jijini Dar Es Salaam katika hafla ya kukabidhi tuzo za umahiri kwa maafisa Habari na Uhusiano zilizoandaliwa na Taasisi ya Public Relations Society of Tanzania(PRST) ambapo Shirika la la Hifadhi ya Taifa Tanzania(TANAPA)kupitia Idara ya Mawasiliano imeshinda tuzo ya Umahiri katika Mawasiliano ya Umma. Aidha amesema Wizara itaendelea kutoa ushirikiano na kwamba wanahitajika Maafisa Uhusiano wa kisasa zaidi ili…

Read More