Author: Mbeya Yetu

Naibu Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka Maafisa Habari nchini kuwa wabunifu,weledi na kufanya kazi kwa uweledi ili kukuza tasnia ya Habari sanjari na kuisaidia serikali katika utendaji wake.

Ameyasema hayo April 5,2024 ukumbi wa St Peters Jijini Dar Es Salaam katika hafla ya kukabidhi tuzo za umahiri kwa maafisa Habari na Uhusiano zilizoandaliwa na Taasisi ya Public Relations Society of Tanzania(PRST) ambapo Shirika la la Hifadhi ya Taifa Tanzania(TANAPA)kupitia Idara ya Mawasiliano imeshinda tuzo ya Umahiri katika Mawasiliano ya Umma.

Aidha amesema Wizara itaendelea kutoa ushirikiano na kwamba wanahitajika Maafisa Uhusiano wa kisasa zaidi ili tasnia hiyo iwe na tija kwa serikali.

Hata hivyo amewataka wasimamizi wa tuzo hizo wasitoe tuzo kwa upendeleo ili vigezo na masharti yazingatiwe.

“Naamini tuzo hizi zitaidia kuboresha kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na waliokosa tuzo wasife moyo bali itawapa ari ya kufanya vizuri mwakani”alisema Mahundi.

Kwa upande wake Mobhali Matinyi Msemaji Mkuu wa Serikali amesema hii ni fursa kwa Maafisa Uhusiano kufanya kazi zao bila kuwategemea Waandishi wa Habari kutoka nje ya ofisi na utaratibu huo utaharakisha utendaji kazi wa kila siku.

Hii ni kazi yake ya kwanza kufanywa na Naibu Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi tangu apate uhamisho kutoka Wizara ya Maji.

Read More

Baadhi ya Wakulima wa Kijiji cha Mbuyuni Kata ya Mapogolo Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamepigwa na wafugaji baada ya wafugaji hao kuadhibiwa na ofisi ya Kijiji kutokana na kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wakulima hao wamedai wafugaji wamekuwa wakiingiza maksudi mifugo kwenye mashamba ya wakulima hali inayowafanya wakulima kuwa hatarini kukumbwa na njaa licha ya mazao yao kustawi vizuri.

Maria Ngajilo mkazi wa Mbuyuni amesema yeye ana wagonjwa wanne nyumbani kwake ambao wanategemea chakula hicho lakini wafugaji hao wameingiza mifugo shambani hivyo kumfanya aishi mazingira magumu.

Naye Veronica Amiri amedai ulezi wake umeliwa na mifugo na alipojaribu kuitoa wakulima walimtishia kumpiga kwa fimbo ambazo wafugaji walikuwa nazo.

Aidha Sandina Ramadhani amesema shamba lake la alizeti nalo limeliwa na kundi la mifugo na alipokwenda kutoa taarifa ofisi ya Kijiji hakupata kusikilizwa.

Eliah Chatila naye ni miongoni mwa waathirika wa wafugaji hao mbali ya mazao yake kuliwa na mifugo amepata ulemavu wa kidole kutokana na kipigo kutoka kwa wafugaji licha ya kutoa taarifa Polisi lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

Chatila amesema alipokuwa akifuatilia suala hilo mahakamani pamoja na matibabu ambayo aligharamia shilingi laki nane akadaiwa kutoa shilingi laki mbili ili kuiondoa kesi mahakamani lakini alitoa shilingi elfu hamsini.

Katika hatua nyingine baadhi ya wachezaji nao wamedai kupigwa na wafugaji hivi karibuni walipokuwa wakicheza mpira uwanja wa Mbuyuni baada ya wafugaji zaidi ya ishirini kuwazingira kwa fimbo uwanjani hapo.

Geaz Onesmo Ngulo mkazi wa Mbuyuni amedai kuvamiwa na wafugaji hao kishwa kurushwa rushwa kichura baada ya wafugaji kutoka ofisi za Kijiji,ambapo Alex Chengula amesema baada ya kupigwa walitoa taarifa ofisi ya Kijiji na Polisi lakini hakuna hatua zozote zilizochukulia kwa wafugaji.

Naye Enock Mwashitete mwakilishi wa wakulima amesema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu ingawa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Kwangula Misana kuulekeza uongozi wa Kijiji na Kata lakini viongozi hao hakuna hatua walizozichukua.

“Tumetenga eneo la malisho Kitongoji cha Mlimani katika matumizi bora ya ardhi lakini eneo hilo halitumiki kama ilivyokusudiwa badala yake wafugaji wanavamia mashamba ya wakulima na kuwapiga”alisema Mwashitete.

Mwashitete amesema kitendo cha Mtendaji Jane Nyudike kufanya kazi katika kituo cha kazi kwa zaidi ya miaka ishirini imekuwa changamoto kwani amekuwa akifanya kazi kwa mazoea ambapo awali alikuwa akiishi kwenye nyumba ya Katibu wa wafugaji hivyo inakuwa ni vigumu kuwasikiliza wakulima pindi wanapoleta malalamiko ofisini.

Kwa upande wake Kazi Mwakasala Mwenyekiti wa wafugaji Kata ya Mapogolo amekiri kuwepo kwa migogoro baina ya wakulima na wafugaji ambapo mara kadhaa amepokea malalamiko kutoka kwa wakulima na amekuwa akifanya vikao vya mara kwa mara na wafugaji.

Mwakasala amesema hivi karibuni amepokea malalamiko kutoka kwa wakulima ambapo wamedai kupigwa na alipofuatilia ofisi ya Kijiji alipata taarifa suala hilo kupelekwa Polisi.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila amesema Wilaya ya Mbarali yenye wakazi zaidi ya laki nne na mifugo zaidi ya laki mbili kwa sasa mgogoro mkubwa katika Wilaya yake ni wakulima na wafugaji hasa baada ya mifugo mingi kuondoshwa katika hifadhi ya Ruaha ambako ndiko ilikuwa sehemu ya malisho yao.

Hata hivyo ameiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wizara ya Kilimo ili kusaidia kuondoa migogoro kutokana na Wilaya ya Mbarali kuwa na mifugo mingi lakini haina hakuna eneo lililotengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo.

Mwila mbali ya kero hiyo amesema kero nyingine ni uvamizi wa wanyama wakali kutoka hifadhi ya Ruaha ambapo wanyama hao hufuata ushoroba kutoka Ruaha kuelekea Mpanga Kipengele,hivi karibuni mwananchi mmoja mkazi wa Igava ameuawa na Simba mwingine amekanyagwa na Tembo amelazwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya akipatiwa matibabu.

Licha ya kuwepo kwa uhuru wa vyombo vya habari baadhi ya watumishi wa Umma bado wanawazuia Waandishi wa Habari kuibua changamoto mbalimbali kama ilivyotokea kwa Polisi Kata ya Mapogolo Sichana Mselemu na Afisa Tarafa ya Rujewa Donald Mwaigombe ambao wanadai Waandishi hawaruhusiwi kufanya kazi bila vibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.

Read More

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila amesema Wilaya ya Mbarali yenye wakazi zaidi ya laki nne na mifugo zaidi ya laki mbili kwa sasa mgogoro mkubwa katika Wilaya yake ni wakulima na wafugaji hasa baada ya mifugo mingi kuondoshwa katika hifadhi ya Ruaha ambako ndiko ilikuwa sehemu ya malisho yao.Baadhi ya Wakulima wa Kijiji cha Mbuyuni Kata ya Mapogolo Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamepigwa na wafugaji baada ya wafugaji hao kuadhibiwa na ofisi ya Kijiji kutokana na kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima. Kwa upande wake Kazi Mwakasala Mwenyekiti wa wafugaji Kata ya Mapogolo amekiri kuwepo kwa…

Read More

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya (MZRH) kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya wameandaa kambi ya kutoa huduma upasuaji kwa watu wenye magonjwa mbalimbali.
Kambi hiyo itahudumiwa kwa ushirikiano wa madaktari bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambao ni wataalamu wa magonjwa ya ubongo, mishipa ya fahamu, saratani pamoja na magonjwa ya mifupa.
Soma zaidi kupitia Mbeya Press Club.

Read More

Watu wawili jinsi ya kike wakazi wa Kiwanja Kata ya Mbugani Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wanadaiwa kuuawa na mtoto mwingine mwenye umri wa miaka sita kujeruhiwa kwa vitu vyenye ncha kali nyumbani kwao.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa aliyeuawa ni mwalimu Herieth Lupembe wa shule ya msingi Mbugani na mwingine ni Ivon Tatizo Haonga(16) mwanafunzi wa kidato cha kwanza sekondari ya lsenyela aliyekuwa anaishi naye.

Taarifa za mauaji hayo zilipatikana jioni machi 30,2024 baada ya mwalimu huyo kutofungua duka lake na simu yake kutopatikana pia kutoonekana kanisani wakati si kawaida yake.

Baadhi ya mashuda wamedai kuwa aliagiza bidhaa za dukani kutoka Mbeya baada ya kutoonekana bidhaa hizo ziliachwa nje ya duka lake lililopo mita hamsini kutoka nyumbani kwake.

Read More

VIJANA wa Kanisa na Kiinjili Afrika Mashariki KKAM kutoka Parishi ya Rwanda Jimbo la Nyanda za Juu kusini Mbeya wamesherekea Sikukuu ya Pasaka kwa kuwakumbuka na kuwatembea watoto yatima na malevi ya watoto wa mitaani katika Kituo cha Mwenye Heri Joseph Kilichomilikiwa na kanisa katoriki Jimbo Kuu ya Mbeya kwa kuwa misaada mbalimbali ya Kibinadamu.

Wakizungumza mara baada ya kukabidhi misaada hiyo Vijana, Wazee wa kanisa pamoja na mchungaji Kutoka Parishi ya Rwanda wamesema msaada huo na utekelezaji wa agizo la Yesu juu ya Upendo huku Msimamizi wa kitup hicho Sista amesema changamoto wanazokabiliwa nazo kwa sasa ni Pampasi za wakubwa hasa kwa vijana wenye changamoto ya ulamavu pamoja na mkaa kwa ajili ya kupikia.

Read More

JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani limeshikilia dreva wa kampuni ya Ahmed Trans lenye namba za Usajili T586 AJH linalofanya safari ya kusafirisha abiria kati ya Mbeya na Tanga Rajab Omari baada ya kumkuta amelewa chakali huku akiwa amebeba abiria tayari ya kwa safari ya kutoka Mbeya kwenda Tanga.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mbeya Mkuu wa Oparesheni ya Trafic kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ACP Nassor Sisiwah amesema wakiwa katika zoezi la ukaguzi wamemkamata Dereva huyo na baada ya kumpima wamemkuta na kileva 450 .3 ml/gm kinyume cha sheria.

ACP Nassor Sisiwah amesema zoezi hilo limelenga pia kufanya ukaguzi wawa magari ambayo yanadaiwa fedha ya Serikali na zoezi litakuwa endelea lakini pia kuwakumbusha wernye vyombo kulipa madeni.

Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya SP Hussen Gawile amesema zoezi ni utaratibu wa kawaida wa Jeshi hilo kufanya ukaguzi ili kuhakikisha wananchi wanakuwa salama wakati wote

Rajabu Ghuliku Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani amesema ukaguzi huo unaonyesha ni jinsi gani Serikali ipo kazini wakati wote huku Dereva Rajab Omary akikiri kuwa amefanya kosa na kwamba hakuwa kwenye ratiba ya safari kwa siku ya leo hivyo amekurupushwa na bosi.

Read More

Watu wawili jinsi ya kike wakazi wa Kiwanja Kata ya Mbugani Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wanadaiwa kuuawa na mtoto mwingine mwenye umri wa miaka miwili kujeruhiwa kwa vitu vyenye ncha kali nyumbani kwao. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa aliyeuawa ni mwalimu Herieth Lupembe wa shule ya msingi Mbugani na mwingine ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza sekondari ya lsenyela aliyekuwa anaishi naye. Taarifa za mauaji hayo zilipatikana jioni machi 30,2024 baada ya mwalimu huyo kutofungua duka lake na simu yake kutopatikana pia kutoonekana kanisani wakati si kawaida yake. Baadhi ya mashuda wamedai kuwa aliagiza bidhaa za dukani kutoka Mbeya…

Read More