Author: Mbeya Yetu

Shirika la kimataifa la HJMRI limesema linatarajia kutoa Sh 500 milioni kuwezesha mabinti balehe na wasichana vijana kupitia mradi wa dreams kwa ufadhiri wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR) Mkurugenzi Mkuu wa HJFMRI Tanzania , Sally Chalamila amesema Machi 16 mwaka huu wilayani Kyela wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa mbalimbali na mashine za kisasa vyenye thamani ya Sh 178 milioni .Mashine na vifaa hivyo vimetolewa na Shirika la HJFMRI kupitia WRAIR -DOD kwa ufadhiri wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani (PEPFAR) kwa kushirikiana na Asasi ya Tumaini.Akizungumza kwa niaba…

Read More

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Kasim Majaliwa Majaliwa tayari amewasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Songwe ulioko Mkoani Mbeya na Kupokelewa na Mwenyeji wake Cde: Juma Z. Homera Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwaajiri ya kushiriki Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani Leo Tarhe18 March 2024 ambalo Kitaifa linafanyika Jijini Mbeya katika Ukumbi wa Eden Highlands Hotel.

Read More

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amemuagiza Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Rebman Ganshonga, kuhakikisha anapeleka huduma ya maji kwenye vitongoji ambavyo bado havina huduma ya maji. Mhandisi Mahundi ametoa maagizo hayo leo Machi 17, 2024 akiwa katika muendelezo wa ziara ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ya kukagua utekelezaji wa miradi ya Maji Mkoani Ruvuma  Akiwa ziarani pia Mhandisi Mahundi ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji ili miradi ya maji iwe endelevu. *WANANCHI ELFU 9,659 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI MALUNGU NYASA* NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi…

Read More

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeitaka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kujidhatiti katika utangazaji utalii ili kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na Utalii nchini. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) ameyasema hayo leo Machi 17,2024 wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Ofisi za Makao Makuu ya TTB jijini Dar es Salaam . TTB YATAKIWA KUJIDHATITI UTANGAZAJI UTALII NCHINI Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeitaka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kujidhatiti katika utangazaji utalii ili kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na Utalii nchini. Mwenyekiti…

Read More

WANANCHI MBEYA WALIA KUVAMIWA NA TAZARA

Wakazi wa Iyunga,Ivumwe,ltuha,ltezi na Nsalaga Jijini Mbeya wameiomba Serikali kutolea ufafanuzi mgogoro wa ardhi baina yao na Shirika la Reli Tanzania na Zambia(TAZARA)baada ya Shirika hilo kuweka mawe(Bicons)katika maeneo yao sanjari na kuwataka wabomoe nyumba zao zinazodaiwa kuwepo mita hamsini ndani ya hifadhi ya reli kinyume na makubaliano.

Wananchi hao kwa nyakati tofauti wakiwa na nyaraka mbalimbali kuhusiana na mgogoro huo wamepaza sauti zao baada ya kugonga ukuta ofisi zote ikiwemo TAZARA na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya.

Read More

Maadhimisho ya wiki ya maji yameanza machi 16,2024 ambayo yatahitimishwa machi 22,2024 kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa Jijini Mbeya na Mbeya Vijijini. Akitoa taarifa ya maadhimisho hayo kwa Waandishi wa Habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Mkurugenzi wa uzalishaji maji na usambazaji maji safi na usafi wa Mazingira Mhandisi Barnabas Konga amesema Wizara ya Maji imekuwa ikiratibu maadhikisho hayo kila mwaka kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa namba 47. Konga ameitaja baadhi ya miradi inayotekelezwa ambapo katika kipindi cha miaka mitatu upatikanaji wa…

Read More

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amemtaka Meneja wa RUWASA Mkoa wa Njombe Mhandisi. Sadick Chakka, kuhakikisha anasimamia wananchi ambao wapo jirani na chanzo cha maji cha Igongwi kilichopo Mkoani humo, wawe wa kwanza kupata huduma ya maji kabla haijafika maeneo mengine yaliyopangwa. Kadhalika ametoa maagizo kwamba mradi huo ukamilike kabla ya tarehe 30 Juni, 2024 ili wananchi waweze kupata huduma ya maji safi na salama. Mahundi ameyasema hayo leo Machi 15, 2024,akiwa Mkoani Njombe kwenye muendelezo wa ziara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji.…

Read More

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhishwa na matumizi ya fedha za mradi wa UVIKO-19 za kuboresha miundombinu ya utalii katika Msitu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi uliogharimu takribani shilingi milioni 579.1 Hayo yamesemwa leo Machi 16, 2024 na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Najma Giga walipofanya ziara ya kukagua miradi iliyotekelezwa na Wakala ya Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika msitu huo. “Kamati imeridhishwa na matumizi ya fedha za UVIKO-19 hasa katika ujenzi wa kituo cha taarifa za utalii, ukiliangalia lina thamani halisi ya…

Read More

Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Chrysoula Zacharopoulou, Waziri wa Nchi-Maendeleo ya Uchumi (Secretary of State for Economic Development) wa Ufaransa. Akizungumza malengo na dhamira ya kutoa mualiko kwa Wizara ya Maji Tanzania, Mheshimiwa Chrysoula amesema Serikali ya Ufaransa inatambua na kuthamini jitihada za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika dhamira ya kuimarisha huduma ya Maji kwa wananchi na kwamba wanaamini hiki ni kipaumbele chake katika kipindi cha uongozi wake na kusisitiza kwamba katika kuunga mkono jitihada hizo serikali yake ya awamu ya sita Serikali ya Ufaransa imejidhatiti kuwekeza katika miradi…

Read More