Author: Mbeya Yetu

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Timotheo Mnzava leo Machi 14, 2024, imetembelea miradi inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufungua utalii wa Malikale kwenye magofu ya Kisiwa cha Kilwa Kisiwani ikiwa ni juhudi mpya za kuongeza zao jipya la utalii huo.

“Tunaposema tunapongeza juhudi za Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kwa vitendo kama hivi. Hapa katika miaka hii mitatu Serikali yake imetoa fedha kuendeleza utalii wa malikale ikiwemo boti mpya ya kisasa ambayo watalii wanaweza kuona ndani ya maji, gati la kushuka abiria, jengo jipya la kufikia abiria na miundombinu mingine ambayo imechagiza idadi ya watalii kuongezeka hapa kutoka wastani wa 2900 hivi hadi 6,400. Haya ndio mafanikio yenye maono,” alisema Mhe. Mnzava.

Ziara hiyo pia walikuwepo Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki, Naibu wake, Mhe. Dunstan Kitandula, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi na watendaji waandamizi kutoka Idara za Wanyamapori, Malikale na Misitu.

Read More

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amemuagiza Mkurugenzi wa Bonde la Rufiji kukutana na kuzungumza na wananchi wanaomiliki maeneo yaliyo nje ya mita 60 kwenye bwawa la Masaka lilipo Mkoani Iringa. Mahundi ametoa maagizo hayo akiwa kwenye muendelezo wa ziara Mkoani humo na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira leo Machi 14 2024 ambapo kamati imetembelea na kukagua ujenzi wa bwawa hilo la Masaka. Akiwa katika ziara hiyo Mhandisi Mahundi pamoja na kamati wameweza kutembelea ujenzi wa bwawa hilo na kuzungumza na wananchi wa vijiji vya Sadani, Makota na Kaning’ombe ambao ni wanufaika wa bwawa hilo…

Read More

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Ombeni Manase Kilawa [43] mkazi wa
Lusese Wilaya ya Mbarali anayetuhumiwa kumuua mke wake aitwaye Happynes
Gervas Mwinuka [40] mkazi wa Kijiji cha Lusese kwa kumkata na kitu chenye ncha kali.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 13, 2024 Kitongoji cha Masista, Kijiji cha
Lusese, Wilaya ya Mbarali baada ya kutokea ugomvi baina ya wana ndoa hao wakiwa
nyumbani kwao na kupelekea mtuhumiwa Ombeni Kilawa kuchukua kisu na kumkata
mke wake shingoni.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi baada
ya mtuhumiwa kumhisi na kumtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
wanaume wengine.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, linatoa wito kwa jamii kuwa pindi wanapopatwa na
tatizo au changamoto katika ndoa zao isiwe suluhisho lake kujichukulia sheria mkononi
bali ni kutafuta ushauri kwa wazazi, walezi, wasimamizi wa ndoa, viongozi wa dini,
katika madawati ya jinsia na watoto waliopo kila Wilaya ya Kipolisi, katika ofisi za
halmashauri au kutafuta haki kwenye Mahakama ili kuepuka madhara.

Read More

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Hamidu Aweso (Mb), leo Tarehe 13 March 2024 Tarehe amewasili Paris nchini Ufaransa na kupokelewa na mwenyeji wake Mhe Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Ali Jabir Mwadini kwa mwaliko maalum wa Benki ya Maendeleo ya Ufaransa (Agence Française de Développement – AFD). Paris-Ufaransa. Waziri wa Maji Mhe Jumaa Hamidu Aweso (Mb), leo Tarehe 13 March 2024 Tarehe amewasili Paris nchini Ufaransa na kupokelewa na mwenyeji wake Mhe Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Ali Jabir Mwadini kwa mwaliko maalum wa Benki ya Maendeleo ya Ufaransa (Agence Française de Développement – AFD). Katika ziara hiyo,…

Read More

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeipongeza Wizara ya Maji kwa utekelezaji wa mradi wa maji wa Itagutwa ambao unahudumiwa jumla ya wananchi 1645 wa Kijiji cha Itagutwa. Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Jackson Kiswaga (Mb) amesema utekelezaji wa mardi huo, utasaidia kutatua changamoto ya maji kwenye Kijiji cha Itagutwa pamoja na baadhi ya vitongoji vilivyopo kwenye vijiji vya Jirani *WIZARA YA MAJI YAIKOSHA KAMATI YA BUNGE KWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI WA ITAGUTWA* KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeipongeza Wizara ya Maji kwa utekelezaji wa mradi wa maji wa Itagutwa…

Read More

Tarehe 06 Machi 2024, Mhe. Phaustine M. Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Maputo alikutana na Balozi wa Jamhuri ya Kenya nchini Msumbiji, Mhe. Philip Githiora kwenye Ofisi za Ubalozi zilizopo Jijini Maputo. Katika mazungumzo yao, Viongozi hao wawili walizungumza masuala ya Ushirikiano baina ya nchi hizi mbili katika sekta mbalimbali. Aidha, walizungumzia masuala yanayohusu Ushirikiano kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kusisitiza haja ya kuimarishwa kwa Jumuiya hiyo kwa maslahi ya Nchi Wanachama Tarehe 06 Machi 2024, Mhe. Phaustine M. Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Maputo alikutana na Balozi wa Jamhuri ya Kenya…

Read More

Mhe. Phaustine M. Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Maputo alikutana na Balozi wa Jamhuri ya Kongo (Congo Brazzaville), Mhe. Constant-Serge Bounda tarehe 11 Machi, 2024 kwenye Ofisi za Ubalozi zilizopo Jijini Maputo. Wakati wa mkutano huo, Viongozi hao wawili walizungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili pamoja na masuala mengine yanayohusu Ushirikiano wa Kikanda. Imetolewa na Ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Maputo 12 Machi, 2024.

Read More

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya imetenga Tsh: Bilioni Nne katika bajeti ya Mwaka huu 2023/24 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Ukerewe Mkoani Mwanza ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya ikiwemo huduma za Kibingwa. Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Machi 13, 2024 wakati wa ziara katika Mkoa wa Mwanza alipoambatana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Stanslaus Nyongo. “Tunamshukuru sana Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan, tunapoelekea Miaka Mitatu ya Rais Samia kwakweli amefanya…

Read More

Jeshi la Polisi Kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo limewataka Wananchi wa Kata ya Endasak Wilaya Hanang Mkoa wa Manyara kuwataja watu wanaojihusisha na wizi wa Mifugo katika eneo hilo huku likiwataka kuwa mstari wa mbele kutoa Ushahidi pindi unapohitajika mahakamani. Hatua hiyo imekuja mara baada ya Kamanda wa kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua wakati alipofika katika mnada wa Endasak uliopo katika Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara ambapo alisikiliza kero za wananchi ambao wanafanya biashara ya mifugo mnadani hapo juu ya kwepo kwa changamoto ya baadhi ya wafanyabiashara wasiowaaminifu.…

Read More

MWALUNENGE AKAGUA MAENDELEO YA UKARABATI UWANJA WA SOKOINE NA KUAHIDI MAKUBWA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge amekagua maendeleo ya ukarabati wa uwanja wa Sokoine kutekeleza agizo la TFF la kuufanyia ukarabati uwanja huo eneo la uwanja na uzio.

Hata hivyo Mwalunenge amebainisha ukarabati mkubwa utafanyika wa kuezeka paa na ufungaji wa taa ili uwanja huo uweze kutumika kwa michezo ya kimataifa hata nyakati za usiku.

Read More