Author: Mbeya Yetu

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya, kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Serikali ya Ujerumani(GIZ), leo tarehe 12/03/2024, wamekabidhi Mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya usafi katika Kata ya Sinde na Shule ya Sekondari ya Sinde. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, mwakilishi wa GIZ Mbeya, Mhandisi Agnes Sigareti, amesema lengo la mradi huu ni kuboresha afya na usafi wa mazingira na kutokomeza magonjwa ya mlipuko katika Kata Sinde kwa kutumia teknolojia rahisi ya kutoa majitaka katika makazi yasiyo na mpangilio rasmi.Mradi huu umegharimu Shilingi milioni 400.6, umelenga maeneo makubwa mawili ambayo ni Uboreshaji wa miundombinu ya Usafi…

Read More

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Misitu na Upandaji miti duniani ambayo kitaifa itafanyika Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Same machi 21 mwaka huu. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu akiwa Wilayani Same kwenye ziara ya kukagua eneo litakalofanyika maadhimisho hayo pamoja na kukagua miradi ya maendeleo atakayotembelea Dkt. Mpango akiwa Wilayani humo. Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wakazi wa Same na maeneo ya jirani kutumia vizuri nafasi ya kuwepo tukio kubwa…

Read More

Na Abel Paul,Jeshi la Polisi- Tinde Shinyanga.

Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo STPU Kimesema Kinawashikilia watuhumiwa kadhaa kwa tuhuma za wizi wa mifugo na utoroshaji Mifugo nje ya nchi huku likisema kuwa litaendelea kushirikiana na wananchi kwa karibu ili kudhibiti uhalifu huo hapa nchini.

Akitoa taarifa hiyo leo Machi 12,2024 na kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo Nchini Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua wakati alipotembelea mnada wa Tinde uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga amesema Jeshi hilo linawashirikilia watuhumiwa wa wizi wa mifugo katika maeneo tofauti tofauti hapa nchini.

Kamanda Pasua ameongeza kuwa watuhumiwa waliokamatwa kwa tuhuma za wizi wa mifugo katika maeneo tofauti hapa nchini majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi ambapo amesema kikosi hicho kitaendelea kuwakamata wale wote watakao bainika katika kujihusisha na wizi wa mifugo.

Aidha amewaomba wananchi kote nchini kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi za baadhi ya watu wanaojihusisha na wizi wa mifugo Pamoja na kutorosha mifugo nje ya nchi.

Kwa upande wake afisa biashara Kutoka Shinyanga vijijini Upendo Milisho amebainisha kuwa wananchi na wafanya biashara mifugo katika mnada wa Tinde uliopo halmashauri ya Shinyanga wamekuwa na mwitikio Chanya katika ulipaji Ushuru kwa kielektroniki mnadani hapo.

Afisa Mapato Wilaya ya Shinyanga Bw. Victor Moleli Pamoja na kushukuru kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo amebainsha kuwa Jeshi la Polisi pamoja na wananchi wameendelea kudhibiti uhalifu katika eneo hilo la mnada wa Tinde kitendo kilichopelekea mnada huo kuwa miongoni mwa minada yenye kukusanya mapato vizuri na usalama wa kutosha.

Read More

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kushirikiana na Taasisi ya 1 New Heart Tanzania inayojihusisha na upimaji wa moyo kwa watoto imewaka kambi ya siku tatu ya uchunguzi na upimaji wa moyo kwa watoto chini ya umri wa miaka 14 kwa wakazi wa Nyanda za Juu Kusini.

Akiongea wakati wa zoezi hilo Dkt. Nuru Mniwa Mkuu wa Idara ya Watoto Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya amesema lengo la kambi hiyo ya siku tatu ni kutoa huduma ya uchunguzi na vipimo kwa watoto chini ya umri wa miaka 14 ili kutambua matatizo mbalimbali ya moyo yanayowakumba pamoja na kuwapuguzia gharama za kusafiri umbali mrefu kwenda kupata huduma hiyo.

“..changamoto kubwa ni uwezekano wa watoto hawa kufika Taasisi ya Moyo ya JKCI pale wanapobainika na tatizo la moyo kutokana na umbali na gharama za kujikimu”.- Dkt. Nuru Mniwa

Kwa upande wake Dkt. Gloria Mbwile, Daktari Bingwa Mbobezi wa magonjwa ya Moyo kwa watoto Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya amesema, magonjwa ya moyo kwa watoto yamegawanyika katika makundi mawili ikwemo magonjwa ya kuzaliwa nayo pamoja na yale yanayoytokana na maambukizi.

Read More

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amejipambanua kama mlezi wa Sekta binafsi nchini na hataki kuona wafanyabiashara wanapata misukosuko wakati wa utekelezaji wa majukumu Amesema maono ya Rais ni kujenga sekta binafsi itakayokuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye pato la Taifa na ili kufikia azma hiyo, viongozi wengine wahakikishe nia njema ya Rais kwa Wafanyabiashara inatekelezwa kwa vitendo.Amesema maono ya Rais ni kujenga sekta binafsi itakayokuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye pato la Taifa na ili kufikia azma hiyo, viongozi wengine wahakikishe nia njema ya Rais kwa Wafanyabiashara…

Read More

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amewataka viongozi wa madhehebu ya kidini Nchini kuendekeza maridhiano ya amani ili kutunza amani na mshikamano uliopo katika Taifa.

Amezungumza hayo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Maridhiano Jijini Mbeya alipomwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye ukumbi wa Hotel ya Tughimbe.

Read More

Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo limesema litaendelea kutoa elimu kwa wafugaji na wafanya biashara wa Mifugo hapa Nchini huku likibainisha kuwa halitomwonea muhali mfugaji yeyote atakaye bainika kutorosha mifugo na kukiuka taratibu za uuzaji wa mifugo hapa nchini. Hayo yamebainisha leo Machi 09, 2024 Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora na Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo hapa nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua alipotembelea mnada wa Upili Igunga ambapo amebainisha kuwa kikosi hicho kitaendelea kutoa elimu kwa wafugaji Nchi nzima ili kuondokana uvunjifu wa sheria.  Wauza mifugo wa Mnada…

Read More