Author: Mbeya Yetu

#mbeyayetutv
Diwani wa kata ya Itezi Sambwee Shitambala amewaita waathirika wa maporomoko ya mlima Kawetere yaliyoathiri kaya 21 za Kata ya Itezi ambao waliweka kambi katika shule ya msingi ya Tambukareli na kuhudhuriwa na viongozi wa CCM na CHADEMA.

Katika kikao hicho viongozi wa CCM na CHADEMA walitupiana makombora wakidai uongozi uliopita chini ya CHADEMA ndio ulioruhusu kugawa viwanja katika maeneo hatarishi.

Read More

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Apimondia Kamisheni ya Afrika, Bw. David Mukomana kwa lengo la kujadili maandalizi ya mkutano wa 50 wa Dunia wa Ufugaji Nyuki (APIMONDIA) na kuweka mikakati ya kufanikisha mkutano huo utakaofanyika nchini mwaka 2027. Akizungumza katika kikao hicho, kilichofanyika leo Aprili 29,2024 jijini Dodoma, Waziri Kairuki amemuhakikishia Bw. Mukomana kuwa Serikali ya Tanzania imejipanga vizuri kufanikisha mkutano huo ikiwemo maandalizi ya ukumbi, utangazaji na masuala mengine ya muhimu. “Nataka niwahakikishie kwamba Tanzania itafanya kazi usiku na mchana kwa ukamilifu, bila kuchoka kwa kushirikiana na uongozi…

Read More

Kaimu Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya UNESCO Tanzania Fatuma Mrope wa kwanza kutoka kulia akikabidhiwa baadhi ya taarifa na Mnufaifaika wa Ufadhili wa Masomo nchini Poland George Kato wa tatu kutoka kushoto katika makabidhiano yaliyofanyika katika Ofisi ya Tume hiyo jijini Dar es Salaam UNESCO Tanzania yataka vijana kuchangamkia fursa za ufadhili wa masomo nje ya nchi -Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu Fatuma *Miradi ya Kimkakati ni fursa ya kwenda kupata ufadhili na kuongeza maarifa Na Mwandishi wetu Vijana nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za kusoma nchi nchi zinazotolewa Tume ya Taifa ya UNESCO kutoka nchi wafadhili. Tume ya…

Read More

Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya imevuka malengo ya makusanyo mapato ya ndani baada ya kukusanya asilimia mia moja arobaini na mbili ikiwa ni ongezeko la asilimia arobaini na mbili hivyo kuongoza kimkoa. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bosco Mwanginde katika kikao cha Baraza ikiwa ni robo ya tatu.Hayo Mwanginde amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Tamim Kambona wafanyakazi wa ldara zote na Madiwani kila mmoja kwa nafasi yake. Mwanginde amewasisitiza watumishi wa Halmashauri pamoja na makusanyo mazuri wazingatie matumizi mazuri ili fedha zirudi kwa wananchi kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya Zahanati,Vituo…

Read More