Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- DKT TULIA ACKSON ASHIRIKI IBADA BAPTIST ISYESYE MADHABAHU YA REHEMA NA SAUTI YA UPONYAJI
- CHADEMA CHUNYA YALIA NA UKOSEFU WA MAGARI POLISI, WAGOMBEA WAFUNGUA KAMPENI
- KUMEKUCHA KAMPENI ZA CCM MBEYA VIJIJINI, MBUNGE NJEZA ASEMA DKT SAMIA KASAFISHA NJIA
- EZEKIA ZAMBI MWENYEKIT ACT WAZALENDO
- CHADEMA LUPA YATUMA SALAMU ZA KUIONDOA CCM IKIZINDUA KAMPENI, KERO ZAAINISHWA
- Huyu mwanamke anadai mimba yangu haionekani tumboni kwake!
- Fedha zangu zote za kustaafu zilikuwa zinateketea hadi nilipoamua kufanya hivi
- POLISI NA WANAHABARI MBEYA WAWEKA MIPANGO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
Author: Mbeya Yetu
Kaimu Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya UNESCO Tanzania Fatuma Mrope wa kwanza kutoka kulia akikabidhiwa baadhi ya taarifa na Mnufaifaika wa Ufadhili wa Masomo nchini Poland George Kato wa tatu kutoka kushoto katika makabidhiano yaliyofanyika katika Ofisi ya Tume hiyo jijini Dar es Salaam UNESCO Tanzania yataka vijana kuchangamkia fursa za ufadhili wa masomo nje ya nchi -Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu Fatuma *Miradi ya Kimkakati ni fursa ya kwenda kupata ufadhili na kuongeza maarifa Na Mwandishi wetu Vijana nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za kusoma nchi nchi zinazotolewa Tume ya Taifa ya UNESCO kutoka nchi wafadhili. Tume ya…
Harusi ya mwana MWEF Wiseman na Mkewe Christine yafana Jijini Mbeya
Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya imevuka malengo ya makusanyo mapato ya ndani baada ya kukusanya asilimia mia moja arobaini na mbili ikiwa ni ongezeko la asilimia arobaini na mbili hivyo kuongoza kimkoa. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bosco Mwanginde katika kikao cha Baraza ikiwa ni robo ya tatu.Hayo Mwanginde amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Tamim Kambona wafanyakazi wa ldara zote na Madiwani kila mmoja kwa nafasi yake. Mwanginde amewasisitiza watumishi wa Halmashauri pamoja na makusanyo mazuri wazingatie matumizi mazuri ili fedha zirudi kwa wananchi kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya Zahanati,Vituo…
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Eng Maryprisca Mahundi (Mb.) alikuwa mgeni rasmi katika Hafla ya siku ya Kimataifa ya Wasichana katika TEHAMA, 2024. Hafla hiyo ilikuwa imeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Hafla hiyo ilishirikisha wanafunzi wa kike kuanzia ngazi ya Awali, Msingi, Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu kutoka Tanzania bara, Unguja na Pemba. Naibu Waziri Mahundi aliipongeza TCRA kwa kuhamasisha ushiriki wa Wasichana katika masuala ya TEHAMA kwa kuwa ni muhimu sana katika kipindi hiki ambapo nchi inaelekea katika Uchumi wa Kidijitali. Aidha, Mhe Naibu Waziri Mahundi alisisitiza watoto wa kike…
#mbeyayetutv
Mke mkubwa wa Mbunge mstaafu wa jimbo la Mbeya mjini Obel Benson Mwamfupe,Bi Sosisyo Kalasya Mwamfupe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90 na kuzikwa nyumbani kwake Lugombo Mwakaleli wilayani Rungwe.
Mwamfupe alipata kuwa Mbunge jimbo la Mbeya mjini kati ya mwaka 1985-1995.
Mtoto mkubwa wa marehemu ambaye ni Meya wa Jiji la Dodoma Prof Davis Obel Mwamfupe amemzungumzia marehemu Mama yake Sosisyo Kalasya Mwamfupe kwamba ukarimu wake ulisababisha nyumbani kwake Lugombo kutopungua wageni mara kwa mara.
Naye Binti wa marehemu Irene Mwamfupe alisema kuwa mama yake mbali ya kuwa ni mzazi wake alikuwa rafiki na msiri wake mkubwa ambaye alikuwa kiunganishi kikubwa cha watoto na familia nzima ya marehemu Obel Mwamfupe.
Leo tarehe 25/4/2024, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Dustan Kyobya na Mkurugenzi wa Ifakara Mji Zahara Michuzi wamefika eneo la kingo za mto lumemo ambao umejaa sana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kuleta mafuriko kwenye makazi na taasisi za umma na binafsi. Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kuchukua tahadhari mapema na kuondoka maeneo yote yaliyojaa maji. Baadhi ya shule zimelazimika kufungwa kwa muda mpaka maji yatakapopungua Timu za uokoaji zimepata boti kutoka TAWA na zinaendelea na doria ya nyumba kwa nyumba kuokoa wananchi. Nyumba nyingi bado zimezungukwa na maji, hivyo timu za uokoaji zikiongozwa na kamanda wa zima…
Makanisa mbalimbali nchini yamekutana Jijini Mbeya kwa lengo la kujadiliana namna ya kuimarisha mahusiano kati ya makanisa na Israel kupitia matukizi ya Teknolojia na utaalamu wa miradi mikubwa ya mazao. Akitoa taarifa kwa wanahabari Mwangalizi Mkuu wa WAPO MISSION INTERNATINAL Profesa Sylvester Gamanywa amesema mradi umeona kuwashirikisha wafanyabiashara Wakristo kutoka Tanzanian katika biashara hizi, kawapa fursa za ubia zinazowiana na dhamira yetu ya kukuza uchumi na maendeleo endelevu. Katika hatua nyingine Gamanywa amesema lengo ni kuunga mkono serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan sanjari na kutoa ajira kwa vijana nchini. Kwa upande…
aasisi ya Tulia Trust imetoa msaada wa vyakula kwa wahanga wa mafuriko yaliyotokea Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kutokana na mvua zinazoendelea Kunyesha hapa nchini.
Vyakula vilivyotolewa na kukabidhiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Josephine Manase ni mchele Kg 300, maharage Kg 50, sukari Kg 75 pamoja na unga wa ugali Kg 125.
Tulia Trust chini ya mkurugenzi wake ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mhe.Dkt. Tulia Ackson inatoa pole kwa wale wote waliokumbwa na Janga hilo la mafuriko.