Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- DKT TULIA ACKSON ASHIRIKI IBADA BAPTIST ISYESYE MADHABAHU YA REHEMA NA SAUTI YA UPONYAJI
- CHADEMA CHUNYA YALIA NA UKOSEFU WA MAGARI POLISI, WAGOMBEA WAFUNGUA KAMPENI
- KUMEKUCHA KAMPENI ZA CCM MBEYA VIJIJINI, MBUNGE NJEZA ASEMA DKT SAMIA KASAFISHA NJIA
- EZEKIA ZAMBI MWENYEKIT ACT WAZALENDO
- CHADEMA LUPA YATUMA SALAMU ZA KUIONDOA CCM IKIZINDUA KAMPENI, KERO ZAAINISHWA
- Huyu mwanamke anadai mimba yangu haionekani tumboni kwake!
- Fedha zangu zote za kustaafu zilikuwa zinateketea hadi nilipoamua kufanya hivi
- POLISI NA WANAHABARI MBEYA WAWEKA MIPANGO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
Author: Mbeya Yetu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Profesa Hamis Malebo Na Mwandishi Wetu Maalum ,Marekani Nchi ya Tanzania umetoa ujumbe wake Kwa Umoja wa Mataifa kuwa haitishi wala kukandamiza raia wake Ujumbe huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Profesa Hamis Malebo kwenye mkutano Jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) ulionza Aprili 15 na kuhitimishwa Aprili 26 unaofanyika nchini Marekani Prof. Malebo ameueleza mkutano huo wa Umoja wa Mataifa kuwa Tanzania nchi inayofuata misingi ya sheria katika mifumo ya kiutawala. “Inasikitikisha kwamba kongamano hilo linatumiwa vibaya kwa…
Taasisi ya Tulia Trust imeanza ujenzi wa nyumba ya Bi. Eliza Yongo Mwaifwani mkazi wa mtaa wa Ilolo kata ya Ruanda Mbeya Mjini kupitia mpango wa Tulia Trust Mtaani Kwetu. Bi.Mwaifwani anaishi na familia yake ya watoto sita katika mazingira magumu na atakabidhiwa nyumba hiyo mapema mwezi Mei mwaka huu. Sambamba na ujenzi huo Tulia Trust inayoongozwa na Mkurugenzi wake ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe.Dr.Tulia Ackson wametoa vifaa vya Shule (Daftari na Sare za Shule) kwa Watoto watatu wa familia hiyo ili…
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera emewataka wananchi wa mkoa wa Mbeya kutambua kuwa mafanikio yaliyopo mkoani Mbeya yanatokana na jitihada zinazofanywa na Rais wa Awamu ya Sita, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ni zao la Muungano. Mhe. Homera ametoa rai hiyo mapema leo tarehe 22 Aprili, 2024 eneo la Uhindini lilipokuwa soko la zamani wakati wa dua ya kuliombea Taifa ikiwa ni sehemu yamaadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ulioasisiwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hayati Sheikh Abeid…
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z .Homera Amesema Serikali Iko tayari kuwapatia Viwanja 21 Waathirika ambao kaya zao zilifukiwa na Udongo mzito uliotokana na Kupasuka kwa Mlima Kawetere ulioko Kata ya Itezi Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Ameyasema hayo Leo alipoupokea Ugeni maalumu Kutoka Ofisi ya Rais Ikulu ukiongozwa na Mshauri wa Rais Maswala ya Siasa na Uhusiano wa Jamii Mh: Wilium Lukuvi(Mb) uliokuja Kutoa Msaada kama Salamu za pole kwa Waathirika hao ambapo Msaada huo umepokelewa na Dkt: Tulia Ackson Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini.
Katika Salamu zake RC Homera Amesema Mh:Rais Dkt:Samia Suluhu Hassan amempa Maagizo hayo kupitia kwa Mshauri wake(Mh: Lukuvi) ambapo naye ameiagiza Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuhakikisha Zoezi hilo linafanyika haraka iwezekanavyo.
#mbeyayetutv
Wafanyabishara na baadhi ya wakazi wa jiji la Mbeya wameendelea kuguswa na kujitokeza kwa wingi kutoa msaada kwa waathirika Maporomoko ya mlima Kawetere katika kata ya itezi jijiini Mbeya
#mbeyayetutv
Kundi la baadhi ya Wafanyabishara wakubwa Jijini Mbeya wanaofahamika kwa jina la Mbeya Real Friends wameguswa na tukio la mafuriko lililoukumba mtaa wa Maanga Veta Kata ya Ilemi Jijini Mbeya na kuchangia msaada wa chakula wenye thamani ya Shilingi milioni 2 kwa Waathirika 23 wa maeneo hayo.
Msaada huo umewasilishwa na Mwenyekiti wa Kundi hilo Francis Msae na kupokelewa na Diwani wa Kata ya Ilemi Angelo Magoma kwa niaba ya wananchi wa maeneo hayo.
#mbeyayetutv
MARY’S WAFANYA MAOMBI KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU
Siku chache baada ya maporomoko ya mlima Kawetere kuathiri wakazi wa kata ya Itezi Jijini Mbeya,Uongozi wa shule ya msingi Mary’s Pre &Primary School umefanya maombi mazito kumshukuru Mwenyezi Mungu kutokana na shule hiyo kunusurika katika maporomoko hayo.