Author: Mbeya Yetu

WANANCHI MBEYA WALIA KUVAMIWA NA TAZARA

Wakazi wa Iyunga,Ivumwe,ltuha,ltezi na Nsalaga Jijini Mbeya wameiomba Serikali kutolea ufafanuzi mgogoro wa ardhi baina yao na Shirika la Reli Tanzania na Zambia(TAZARA)baada ya Shirika hilo kuweka mawe(Bicons)katika maeneo yao sanjari na kuwataka wabomoe nyumba zao zinazodaiwa kuwepo mita hamsini ndani ya hifadhi ya reli kinyume na makubaliano.

Wananchi hao kwa nyakati tofauti wakiwa na nyaraka mbalimbali kuhusiana na mgogoro huo wamepaza sauti zao baada ya kugonga ukuta ofisi zote ikiwemo TAZARA na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya.

Read More

Maadhimisho ya wiki ya maji yameanza machi 16,2024 ambayo yatahitimishwa machi 22,2024 kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa Jijini Mbeya na Mbeya Vijijini. Akitoa taarifa ya maadhimisho hayo kwa Waandishi wa Habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Mkurugenzi wa uzalishaji maji na usambazaji maji safi na usafi wa Mazingira Mhandisi Barnabas Konga amesema Wizara ya Maji imekuwa ikiratibu maadhikisho hayo kila mwaka kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa namba 47. Konga ameitaja baadhi ya miradi inayotekelezwa ambapo katika kipindi cha miaka mitatu upatikanaji wa…

Read More

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amemtaka Meneja wa RUWASA Mkoa wa Njombe Mhandisi. Sadick Chakka, kuhakikisha anasimamia wananchi ambao wapo jirani na chanzo cha maji cha Igongwi kilichopo Mkoani humo, wawe wa kwanza kupata huduma ya maji kabla haijafika maeneo mengine yaliyopangwa. Kadhalika ametoa maagizo kwamba mradi huo ukamilike kabla ya tarehe 30 Juni, 2024 ili wananchi waweze kupata huduma ya maji safi na salama. Mahundi ameyasema hayo leo Machi 15, 2024,akiwa Mkoani Njombe kwenye muendelezo wa ziara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji.…

Read More

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhishwa na matumizi ya fedha za mradi wa UVIKO-19 za kuboresha miundombinu ya utalii katika Msitu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi uliogharimu takribani shilingi milioni 579.1 Hayo yamesemwa leo Machi 16, 2024 na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Najma Giga walipofanya ziara ya kukagua miradi iliyotekelezwa na Wakala ya Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika msitu huo. “Kamati imeridhishwa na matumizi ya fedha za UVIKO-19 hasa katika ujenzi wa kituo cha taarifa za utalii, ukiliangalia lina thamani halisi ya…

Read More

Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Chrysoula Zacharopoulou, Waziri wa Nchi-Maendeleo ya Uchumi (Secretary of State for Economic Development) wa Ufaransa. Akizungumza malengo na dhamira ya kutoa mualiko kwa Wizara ya Maji Tanzania, Mheshimiwa Chrysoula amesema Serikali ya Ufaransa inatambua na kuthamini jitihada za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika dhamira ya kuimarisha huduma ya Maji kwa wananchi na kwamba wanaamini hiki ni kipaumbele chake katika kipindi cha uongozi wake na kusisitiza kwamba katika kuunga mkono jitihada hizo serikali yake ya awamu ya sita Serikali ya Ufaransa imejidhatiti kuwekeza katika miradi…

Read More

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Timotheo Mnzava leo Machi 14, 2024, imetembelea miradi inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufungua utalii wa Malikale kwenye magofu ya Kisiwa cha Kilwa Kisiwani ikiwa ni juhudi mpya za kuongeza zao jipya la utalii huo.

“Tunaposema tunapongeza juhudi za Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kwa vitendo kama hivi. Hapa katika miaka hii mitatu Serikali yake imetoa fedha kuendeleza utalii wa malikale ikiwemo boti mpya ya kisasa ambayo watalii wanaweza kuona ndani ya maji, gati la kushuka abiria, jengo jipya la kufikia abiria na miundombinu mingine ambayo imechagiza idadi ya watalii kuongezeka hapa kutoka wastani wa 2900 hivi hadi 6,400. Haya ndio mafanikio yenye maono,” alisema Mhe. Mnzava.

Ziara hiyo pia walikuwepo Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki, Naibu wake, Mhe. Dunstan Kitandula, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi na watendaji waandamizi kutoka Idara za Wanyamapori, Malikale na Misitu.

Read More

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amemuagiza Mkurugenzi wa Bonde la Rufiji kukutana na kuzungumza na wananchi wanaomiliki maeneo yaliyo nje ya mita 60 kwenye bwawa la Masaka lilipo Mkoani Iringa. Mahundi ametoa maagizo hayo akiwa kwenye muendelezo wa ziara Mkoani humo na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira leo Machi 14 2024 ambapo kamati imetembelea na kukagua ujenzi wa bwawa hilo la Masaka. Akiwa katika ziara hiyo Mhandisi Mahundi pamoja na kamati wameweza kutembelea ujenzi wa bwawa hilo na kuzungumza na wananchi wa vijiji vya Sadani, Makota na Kaning’ombe ambao ni wanufaika wa bwawa hilo…

Read More

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Ombeni Manase Kilawa [43] mkazi wa
Lusese Wilaya ya Mbarali anayetuhumiwa kumuua mke wake aitwaye Happynes
Gervas Mwinuka [40] mkazi wa Kijiji cha Lusese kwa kumkata na kitu chenye ncha kali.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 13, 2024 Kitongoji cha Masista, Kijiji cha
Lusese, Wilaya ya Mbarali baada ya kutokea ugomvi baina ya wana ndoa hao wakiwa
nyumbani kwao na kupelekea mtuhumiwa Ombeni Kilawa kuchukua kisu na kumkata
mke wake shingoni.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi baada
ya mtuhumiwa kumhisi na kumtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
wanaume wengine.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, linatoa wito kwa jamii kuwa pindi wanapopatwa na
tatizo au changamoto katika ndoa zao isiwe suluhisho lake kujichukulia sheria mkononi
bali ni kutafuta ushauri kwa wazazi, walezi, wasimamizi wa ndoa, viongozi wa dini,
katika madawati ya jinsia na watoto waliopo kila Wilaya ya Kipolisi, katika ofisi za
halmashauri au kutafuta haki kwenye Mahakama ili kuepuka madhara.

Read More

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Hamidu Aweso (Mb), leo Tarehe 13 March 2024 Tarehe amewasili Paris nchini Ufaransa na kupokelewa na mwenyeji wake Mhe Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Ali Jabir Mwadini kwa mwaliko maalum wa Benki ya Maendeleo ya Ufaransa (Agence Française de Développement – AFD). Paris-Ufaransa. Waziri wa Maji Mhe Jumaa Hamidu Aweso (Mb), leo Tarehe 13 March 2024 Tarehe amewasili Paris nchini Ufaransa na kupokelewa na mwenyeji wake Mhe Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Ali Jabir Mwadini kwa mwaliko maalum wa Benki ya Maendeleo ya Ufaransa (Agence Française de Développement – AFD). Katika ziara hiyo,…

Read More