Author: Mbeya Yetu

*MH:FESTO SANGA AWALILIA WATUMISHI NCHINI, RIBA ZA MABENKI ZINAWAUMIZA*

Mbunge wa Makete Mh:Festo Sanga amepaza leo tar 14:02:2024 akichangia hoja ya Kamati ya Bajeti amepaza kilio chake kwa serikali namna mabenki nchini yanavyoumiza watumishi kwenye riba za mikopo.
Sanga amesema ” Uhai wa benki zetu nchini zinabebwa na Watumishi,lakini kiwango cha riba wanachotozwa wanapokopa ni kikubwa sanaa kinyume na uhalisia, riba hizo zimegeuka mwiba mchungu kwa watumishi wetu wazalendo hapa nchini, Benki hizi zinapata riba ndogo wanapokopa Benki Kuu, lakini wao wanatoza riba kwa watumishi bila kujali mchango wao kwenye uhai wa hizo benki,”

Anaendelea “Bank nyingi zinapata faida kwa “Horizontal gain” hawahanagiki kwenda kutafuta wateja wengine ambao waangesaidia kuongeza mzunguko wa fedha kwenye mabenki na kuwapunguzia mzigo watumishi, kila jicho la benki linaangalia namna ya kupata faida kwa mtumishi aidha kwa makato au kwa riba kwenye mikopo, kwanini hawajawekeza kwenye Rural banking? Watanzania wengi wanafedha huko vijijini lakini hawana elimu ya benki”.

Mwisho ameshauri “Gavana kupitia Benki kuu kupitia upya mchakato wa mabanki yanavyopanga riba, vilevile waziri wa fedha aunde kikosi kazi kufuatilia microfinance zinazotoza riba kinyume na utaratibu”.

Read More