Author: Mbeya Yetu

MABILIONI YA MAMA SAMIA YAWAKIMBIZA WASOMI MUST.

Wanafunzi wa chuo Cha sayansi na teknolojia Mbeya MUST wamekimbia zaidi ya kilomita 12, kwa mbio za polepole, ikiwa ni sehemu ya kutambua na kupongeza uwekezaji unaofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kuboresha miundombinu mbalimbali ya Elimu katika chuo hicho.

Wakizungumza baada ya kuhitimisha mbio hizo viongozi wa Serikali ya wanafunzi kutoka chuo hicho (MUSTSO) wamesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, inatekeleza miradi ya zaidi ya Billioni 36 katika ujenzi wa majengo mbalimbali ya utawala na hostel katika chuo hicho, itakayo saidia wanafunzi kupata elimu Bora baada ya miradi hiyo kukamilika.

Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama Cha mapinduzi UVCCM Mkoa wa Mbeya Yasin Ngonyani, amesema wao kama chama wataendelea kuishauri serikali kuendelea kuwekeza katika secta ya Elimu Ili kupambana na adui Ujinga katika kizazi Cha Sasa na baadae.

Read More