Author: Mbeya Yetu

Ujenzi barabara ya Lupeta-Wimba-Izumbwe kuinua Uchumi wa wananchi Mbeya.

Mbeya

Ujenzi wa barabara ya Lupeta-Wimba -Izumbwe yenye urefu wa Km.9.5 na ile ya Inyala-Simambwe Km. 16.7 kwa kiwango cha lami imelenga kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi mkoani Mbeya kwa kurahisisha usafirishaji wa mazao kwa urahisi.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Dennis Londo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya elimu na miundombinu ya Barbara mkoani Mbeya.

Mhe. Lundo alisema kuwa kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja chini ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

“Kazi kubwa na yenye viwango imefanyika katika elimu na miundombinu katika Halmashauri hii, Miradi hii miwili ya barabara tuliyotembelea ni muhimu kwa uchumi wa Mbeya lakini na Taifa kwa ujumla”Alisema Mhe. Londo

Kwa upande wa uchumi Mhe. Londo alisema barabara hizo zitaeda kurahisisha shughuli za kilimo na kupunguza gharama za pembejeo na uzalishaji kwani gharama za usafirishaji zitapungua, hivyo kumuongezea kipato mkulima mmoja mmoja na kumuondolea umaskini mwananchi.

Read More