Author: Mbeya Yetu

#MbeyaYetuTv
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert John Chalamila ametoa masaa 7 na kuwataka wadaiwa Sugu wa Ranchi ya Taifa ya NARCO iliyopo Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya kulipa madeni yao zaidi ya Shilingi Bil.1.7.
Chalamila amesema Wadaiwa hao Sugu akiwemo aliyekuwa Waziri wa Fedha Basil Mramba,aliyekuwa Mbunge wa Mbarali Esterina Kilasi na baadhi ya Wafanyabiashara wanatakiwa kulipa fedha hizo ndani ya saa 7 ambapo pia amesema mara baada ya tamko hilo, mifugo ya wafanyabiashara hao itakuwa chini ya mikono ya serikali hadi hapo watakapolipa deni hilo.

Read More