Author: Mbeya Yetu

#MbeyaYetuTv
Mfanyabiashara mkubwa wa Madini aina ya dhahabu wilayani Chunya mkoani Mbeya amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya pamoja na wafanyabiashara wenzie wanne wakikabiliwa na kosa la uhujumu wa Uchumi, Kutakatisha fedha, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kupatikana na Madini aina ya Dhahabu kinyume cha sheria,.

Read More

#MbeyaYetuTv
Sakata la watuhumiwa wa mauaji ya mkazi wa Chunya Tenson Ndege Meta,kudaiwa kuachiwa huru, limechukua sura mpya baada ya Kaimu Mkuu wa Mashtaka mkoa wa Mbeya Basilius Namkambe kutoa msimamo wake na kuelezea namna taarifa zilizomo kwenye jalada la Daktari zinavyotofautiana na taarifa zinazodaiwa kuelezwa na ndugu wa marehemu,
Wakili Msomi Namkambe amesema kuwa anashangazwa na taarifa zinazodaiwa na wanandugu kufukuzwa wakati wa kufanyiwa uchunguzi mwili wa marehemu ilhali katika taarifa iliyowasilishwa na Daktari aliyefanya uchunguzi zimemuandika mmoja wa mashuhuda kuwa ni mke wa marehemu Rehema Daimon.l

Read More

#MbeyaYetuTv
Imeelezwa kuwa Watuhumiwa wanne wa mauaji ya mkazi wa Chunya mkoani Mbeya Tenson Ndege Meta wameachiwa huru .
Taarifa kutoka kwa wanafamilia akiwemo mke wa marehemu Rehema Daimon, dada wa marehemu Mage Ndege Meta na mjomba wa marehemu William Mgawe wanasimulia mkasa mzima wa tukio la mauaji na mazingira yenye utata ya kuachiwa huru kwa watuhumiwa hao wa mauaji.

Read More