Browsing: Video Mpya

#mbeyayetutv
Diwani wa kata ya Itezi Sambwee Shitambala amewaita waathirika wa maporomoko ya mlima Kawetere yaliyoathiri kaya 21 za Kata ya Itezi ambao waliweka kambi katika shule ya msingi ya Tambukareli na kuhudhuriwa na viongozi wa CCM na CHADEMA.

Katika kikao hicho viongozi wa CCM na CHADEMA walitupiana makombora wakidai uongozi uliopita chini ya CHADEMA ndio ulioruhusu kugawa viwanja katika maeneo hatarishi.

#mbeyayetutv
Mke mkubwa wa Mbunge mstaafu wa jimbo la Mbeya mjini Obel Benson Mwamfupe,Bi Sosisyo Kalasya Mwamfupe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90 na kuzikwa nyumbani kwake Lugombo Mwakaleli wilayani Rungwe.

Mwamfupe alipata kuwa Mbunge jimbo la Mbeya mjini kati ya mwaka 1985-1995.

Mtoto mkubwa wa marehemu ambaye ni Meya wa Jiji la Dodoma Prof Davis Obel Mwamfupe amemzungumzia marehemu Mama yake Sosisyo Kalasya Mwamfupe kwamba ukarimu wake ulisababisha nyumbani kwake Lugombo kutopungua wageni mara kwa mara.

Naye Binti wa marehemu Irene Mwamfupe alisema kuwa mama yake mbali ya kuwa ni mzazi wake alikuwa rafiki na msiri wake mkubwa ambaye alikuwa kiunganishi kikubwa cha watoto na familia nzima ya marehemu Obel Mwamfupe.

aasisi ya Tulia Trust imetoa msaada wa vyakula kwa wahanga wa mafuriko yaliyotokea Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kutokana na mvua zinazoendelea Kunyesha hapa nchini.

Vyakula vilivyotolewa na kukabidhiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Josephine Manase ni mchele Kg 300, maharage Kg 50, sukari Kg 75 pamoja na unga wa ugali Kg 125.

Tulia Trust chini ya mkurugenzi wake ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mhe.Dkt. Tulia Ackson inatoa pole kwa wale wote waliokumbwa na Janga hilo la mafuriko.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z .Homera Amesema Serikali Iko tayari kuwapatia Viwanja 21 Waathirika ambao kaya zao zilifukiwa na Udongo mzito uliotokana na Kupasuka kwa Mlima Kawetere ulioko Kata ya Itezi Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Ameyasema hayo Leo alipoupokea Ugeni maalumu Kutoka Ofisi ya Rais Ikulu ukiongozwa na Mshauri wa Rais Maswala ya Siasa na Uhusiano wa Jamii Mh: Wilium Lukuvi(Mb) uliokuja Kutoa Msaada kama Salamu za pole kwa Waathirika hao ambapo Msaada huo umepokelewa na Dkt: Tulia Ackson Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini.

Katika Salamu zake RC Homera Amesema Mh:Rais Dkt:Samia Suluhu Hassan amempa Maagizo hayo kupitia kwa Mshauri wake(Mh: Lukuvi) ambapo naye ameiagiza Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuhakikisha Zoezi hilo linafanyika haraka iwezekanavyo.