Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- Afichua siri ya kunusurika katika ajali iliyoua watu 56
- MBUNGE SONGWE PHILIPO MULUGO ANAVYOJIVUNIA UWEKEZAJI WA MABILIONEA WA DHAHABU JIMBONI KWAKE
- UFUNGUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA MKOANI MBEYA
- BILIONEA WA DHAHABU FREDDY ASHERY WILAYANI SONGWE, MKOPO WA BIL 10 ZA NMB ZILIVYOMPA ”KICK”
- Wezi waliopora Mzee Ksh200,000 washindwa kutembea na kuganda kama sanamu!
- WATAALAMU WA HOSPITALI YA KANDA MBEYA WAWASILI CHUNYA KWENYE KAMBI YA MATIBABU YA MTOTO WA JICHO, ZAIDI YA WAGONJWA 500 KUNUFAIKA KAMBI HIYO.
- Nimemtafutia mpenzi wangu kazi sasa kanizidi mshahara
- CPA Gilbert Kayange Akagua Miradi na Kusikiliza Changamoto za Wateja Mbeya
Browsing: Video Mpya
Ibada ya Mbaraka kwa Askofu Mteule Robert Pangani wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi itafanyika Juni 2,2024 Viwanja vya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji Jijini Mbeya.
Akitoa taarifa kwa Wanahabari Makamu Askofu Kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania Askofu Kenani Panja amesema mgeni Rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Israel Mwakilasa amesema mbali ya Rais wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wamealikwa kuhudhuria hafla hiyo.
Askofu Mteule Robert Pangani atakuwa Askofu wa tatu kushika nafasi hiyo baada ya watangulizi Askofu Yohana Wavenza na Askofu Alinikisa Cheyo.
TAASISI YA MARYPRISCA WOMEN EMPOWERMENT FUNDATION YATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAPOROMOKO YA MLIMA
Maandiko matakatifu katika kitabu cha Biblia Yakobo 1:27 yanasema Dini safi ni kuwaona yatima,wajane na watu wenye uhitaji wakati Korani takatifu Sura ya 4 aya ya 36 inasema thawabu kwa Waislam ni kutoa sadaka kwa watu walio katika dhiki.
Hivi ndivyo Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation(MWEF)inayoongozwa Mhandisi Maryprisca Mahundi Naibu Waziri wa Habari Teknolojia ya Mawasiliano na Habari Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya ambaye ndiye Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Mhandisi Maryprisca Mahundi ilivyojitokeza kutoa msaada kwa waathirika wa maporomoko ya mlima Kawetere Kata ya Itezi Jijini Mbeya.
Baraka Mlonga ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation(MWEF)amesema Mkurugenzi wake Mhandisi Maryprisca Mahundi alitamani kuwepo lakini yupo nje ya nchi hivyo wapokee msaada huo na uwe faraja kwa waathirika.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Itezi Sambwee Shitambala mbali ya kushukuru kupokea msaada huo ameomba wasisisite kurudi tena kwani bado msaada unahitajika zaidi
Rais wa chama cha walimu Tanzania CWT Leah Ulaya ameikumusha serikali juu ya upandishwaji wa madaraja kwa walimu kutokana na baadhi ya walimu nchini kukaa kwenye nafasi moja kwa muda mrefu hali ambayo inapunguza ufanisi wa ufanyaji kazi kitaaluma
Rai hiyo imetolewa mala baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa 10 wa Mwaka ukiwahusisha umoja wa maafisa Elimu wa mikoa na Wilaya
Aidha katibu wa chama cha walimu CWT Joseph Msalaba amesema mara baada ya mafunzo wanayo yapata maafisa Elimu katika mkutano huo utakao dumu kwa muda wa siku 5 mafunzo yanayo fanyikia mkoani Mbeya utakuwa na manufaa makubwa yatakayo leta manufaa katika sekta ya Elimu nchini
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde Juma Z. Homera amefika Mlima Kawetele uliopolomoka Alfajiri ya Leo na Kusababisha Kufukiwa kwa Nyumba 20, Ng’ombe Wanne na Kuharibika kwa Miundombinu ya Shule ya Mary’s katika Mtaa wa Gombe Kata ya Itezi Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Akizungumza baada Kuwasili eneo la Tukio RC Homera amekanusha Uvumi unaozagaa Mtandaoni ukidai Kuna Maafa katika tukio hilo ambapo amesema zaidi ya hivyo vilivyotajwa Aya ya Kwanza hakuna Madhara mengine Wala Maafa kama inavyoripotiwa na Baadhi ya Watu.
Aidha Homera ameiagiza Halmashauri ya Jiji la Mbeya kufanya Tathimini juu ya Waathirika hasa wale wasio na Malazi ya Kulala wahakikishe wanapatiwa Sehemu hizo wakati huu ambao Serikali inaendelea kupambana kuhakikisha Hali inakuwa Sawa katika Maeneo hayo.
Pia amekiagiza Kitengo Cha Ardhi Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuacha kuwapimia Wananchi Viwanja eneo lenye Changamoto hasa ya Mkondo wa Maji kwa kufanya Kwao hivyo kutasababisha Matatizo kama hayo ambayo yangeweza kuzuilika.
Tukio hilo limetokea Alfajiri ya Kuamkia Leo ambapo chanzo Chake ni Mvua zinazoendelea Kunyesha Mfululizo na Matukio yanayofanana na haya yamekuwa yakitukia Mikoa Mbalimbali ikiwemo Mikoa ya Arusha na Lindi.
Wananchi wa kata ya Nzovwe na Mabatini jijini Mbeya wameiomba serikali kuwalipa fidia ya kuwasimamisha uendelezaji wa makazi yao na shughuli nyingine za kiuchumi kwa zaidi ya miaka kumi na mbili baada ya mabadiliko ya sheria ya hifadhi za barabara ya kuongeza mita saba mbele kutoka mita 22.5 za awali.
Wananchi wamepaza kilio hicho kwa serikali na kuiomba kuwalipa fidia baada ya kuwakataza kuendeleza makazi yao kwa ajiri ya hifadhi ya barabara ambapo wamedai walifanyiwa tathimini ya nyumba zao toka mwaka 2012 na kwa sasa hawana matumaini ya kulipwa kutokana na mabadiliko yaliyojitokeza.
Timu ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Patrick Mwalunenge kwa kushrikiana na ofisi ya Meneja wa TANROADs mkoa wa Mbeya wamefika eneo lenye mgogoro ili kujionea hali halisi na maelekezo ya chama kwa wananchi.
Waumini wa Kanisa la Gofan Wajitokeza Kufanya Usafi kwenye Eneo Wanaloamini Ni Mali Yao Jijini Mbeya
Mgogoro wa uwanja wa Kanisa la Gofan na Jiji umechukua sura mpya baada ya Kanisa hilo kugoma kwenda mahakamani kama walivyoshauriwa na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson Kanisa likidai mgogoro ulikwisha.
Kikao cha mwisho kilichofanyika hivi karibuni ambacho kilihudhuriwa na Dkt Tulia Ackson na kuzisikiliza pande zote ambapo alilishauri Kanisa kwenda mahakamani ili Kanisa liweze kupata haki yake.
Siku chache baada ya ushauri huo Mchungaji John Ikowelo na waumini wake wamejitokeza kufanya usafi eneo linalogombaniwa ambapo Mchungaji amesema yeye hawezi kuishitaki serikali kwani serikali imemfanyia mambo mengi na ilimaliza kabisa mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi.
Nao baadhi ya waumini wamesema mgogoro umekwisha wanachosubiria ni kibali cha ujenzi ambacho Jiji wanasita kuwapatia kwa muda mrefu hivyo wameamua kufanya usafi kwenye uwanja wao ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa Kanisa.
Mgogoro umedumu kwa zaidi ya miaka kumi ambapo kila upande unadai hilo ni eneo lake Jiji wakidai ni la shule ni eneo oevu halipaswi kujengwa nyumba huku Kanisa likidai eneo ni halali yao.