Browsing: Video Mpya

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Ombeni Manase Kilawa [43] mkazi wa
Lusese Wilaya ya Mbarali anayetuhumiwa kumuua mke wake aitwaye Happynes
Gervas Mwinuka [40] mkazi wa Kijiji cha Lusese kwa kumkata na kitu chenye ncha kali.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 13, 2024 Kitongoji cha Masista, Kijiji cha
Lusese, Wilaya ya Mbarali baada ya kutokea ugomvi baina ya wana ndoa hao wakiwa
nyumbani kwao na kupelekea mtuhumiwa Ombeni Kilawa kuchukua kisu na kumkata
mke wake shingoni.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi baada
ya mtuhumiwa kumhisi na kumtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
wanaume wengine.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, linatoa wito kwa jamii kuwa pindi wanapopatwa na
tatizo au changamoto katika ndoa zao isiwe suluhisho lake kujichukulia sheria mkononi
bali ni kutafuta ushauri kwa wazazi, walezi, wasimamizi wa ndoa, viongozi wa dini,
katika madawati ya jinsia na watoto waliopo kila Wilaya ya Kipolisi, katika ofisi za
halmashauri au kutafuta haki kwenye Mahakama ili kuepuka madhara.

MWALUNENGE AKAGUA MAENDELEO YA UKARABATI UWANJA WA SOKOINE NA KUAHIDI MAKUBWA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge amekagua maendeleo ya ukarabati wa uwanja wa Sokoine kutekeleza agizo la TFF la kuufanyia ukarabati uwanja huo eneo la uwanja na uzio.

Hata hivyo Mwalunenge amebainisha ukarabati mkubwa utafanyika wa kuezeka paa na ufungaji wa taa ili uwanja huo uweze kutumika kwa michezo ya kimataifa hata nyakati za usiku.

Na Abel Paul,Jeshi la Polisi- Tinde Shinyanga.

Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo STPU Kimesema Kinawashikilia watuhumiwa kadhaa kwa tuhuma za wizi wa mifugo na utoroshaji Mifugo nje ya nchi huku likisema kuwa litaendelea kushirikiana na wananchi kwa karibu ili kudhibiti uhalifu huo hapa nchini.

Akitoa taarifa hiyo leo Machi 12,2024 na kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo Nchini Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua wakati alipotembelea mnada wa Tinde uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga amesema Jeshi hilo linawashirikilia watuhumiwa wa wizi wa mifugo katika maeneo tofauti tofauti hapa nchini.

Kamanda Pasua ameongeza kuwa watuhumiwa waliokamatwa kwa tuhuma za wizi wa mifugo katika maeneo tofauti hapa nchini majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi ambapo amesema kikosi hicho kitaendelea kuwakamata wale wote watakao bainika katika kujihusisha na wizi wa mifugo.

Aidha amewaomba wananchi kote nchini kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi za baadhi ya watu wanaojihusisha na wizi wa mifugo Pamoja na kutorosha mifugo nje ya nchi.

Kwa upande wake afisa biashara Kutoka Shinyanga vijijini Upendo Milisho amebainisha kuwa wananchi na wafanya biashara mifugo katika mnada wa Tinde uliopo halmashauri ya Shinyanga wamekuwa na mwitikio Chanya katika ulipaji Ushuru kwa kielektroniki mnadani hapo.

Afisa Mapato Wilaya ya Shinyanga Bw. Victor Moleli Pamoja na kushukuru kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo amebainsha kuwa Jeshi la Polisi pamoja na wananchi wameendelea kudhibiti uhalifu katika eneo hilo la mnada wa Tinde kitendo kilichopelekea mnada huo kuwa miongoni mwa minada yenye kukusanya mapato vizuri na usalama wa kutosha.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kushirikiana na Taasisi ya 1 New Heart Tanzania inayojihusisha na upimaji wa moyo kwa watoto imewaka kambi ya siku tatu ya uchunguzi na upimaji wa moyo kwa watoto chini ya umri wa miaka 14 kwa wakazi wa Nyanda za Juu Kusini.

Akiongea wakati wa zoezi hilo Dkt. Nuru Mniwa Mkuu wa Idara ya Watoto Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya amesema lengo la kambi hiyo ya siku tatu ni kutoa huduma ya uchunguzi na vipimo kwa watoto chini ya umri wa miaka 14 ili kutambua matatizo mbalimbali ya moyo yanayowakumba pamoja na kuwapuguzia gharama za kusafiri umbali mrefu kwenda kupata huduma hiyo.

“..changamoto kubwa ni uwezekano wa watoto hawa kufika Taasisi ya Moyo ya JKCI pale wanapobainika na tatizo la moyo kutokana na umbali na gharama za kujikimu”.- Dkt. Nuru Mniwa

Kwa upande wake Dkt. Gloria Mbwile, Daktari Bingwa Mbobezi wa magonjwa ya Moyo kwa watoto Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya amesema, magonjwa ya moyo kwa watoto yamegawanyika katika makundi mawili ikwemo magonjwa ya kuzaliwa nayo pamoja na yale yanayoytokana na maambukizi.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amewataka viongozi wa madhehebu ya kidini Nchini kuendekeza maridhiano ya amani ili kutunza amani na mshikamano uliopo katika Taifa.

Amezungumza hayo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Maridhiano Jijini Mbeya alipomwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye ukumbi wa Hotel ya Tughimbe.

Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi- Arusha
Ikiwa leo ni Machi 08,2024 kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani, Mtaandao wa
Polisi Wanawake Mkoa wa Arusha wameunga na wanawake wengine Mkoani humo huku
Mtandao huo wakiitumia siku hiyo kuwawekea akiba ya fedha katika mfuko wa uwekezaji (UTT)
kwa Watoto wawili wa askari wanandoa waliofariki kwa ajali ya gari.
Akiongea katika Viwanja vya Ngarenaro Complex Jijini Arusha Mwenyekiti wa Mtandao huo
Mkoa wa Arusha Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema mtaandao huo
katika kuelekea kilele hicho ulianza mapema kutoa elimu maeneo mbalimbali Pamoja na
kufanya ibada ya kuwaombea marehemu.
SSP Zauda ameongeza kuwa katika kuadhimisha siku hiyo waliona vyema kuunga na
kuwawekea akiba ya fedha kwa Watoto wa askari wanandoa waliofariki katika ajali ya gari
ambapo amebainisha kuwa fedha hizo zitawasaidia Watoto hao katika swala la elimu na
mahitaji mengine ya kibinadamu.
Aidha ametoa wito kwa wanawake wengine Mkoani humo kufanya kazi kwa bidii,nidhamu na
kutenda haki ili ustawi bora na wajikwamue kiuchumi na maendeleo ya Taifa kwa Ujumla.
Nae mrakibu msaidizi wa Polisi Lucy Teesa kutoka Makao Makuu ya kikosi cha Kuzuia wizi wa
Mifugo STPU amewaomba wanaweka wenzake kushiriki vyema katika mapambano dhidi
uhalifu ambapo amewaomba kutoa taarifa za uhalifu na kujikitaa katika malezi bora ya Watoto
ili kujenga Jamii iliyostarabika.
Kwa upande wake Mkuu wa kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi Murieti Mrakibu msaidizi wa Polisi
ASP Tausi Mbalamwezi amewaomba wanawake wenzake kujiamini na kujituma katika
kutekeleza majukumu yao huku akiwaomba kuumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuliinua taifa kiuchumi.

#mbeyayetutv

Miaka 8 ya Jumuiya ya Maridhiano na Amani JMAT ilivyoadhimisha Wilayani Kyela.

Mkuu wa Wilaya ya Kyela Josephine Manase amesema Wilaya ya Kyela imeadhimisha Kitaifa Maridhiano Day kwa kuendesha ligi Maalumu ya Kombe la (Samia Maridhiano Cup)ambalo limefikia kilele kwa michuano ya soka.

DC Manase amesema michezo hiyo ya Samia Maridhiano Amani Cup limeacha ujumbe wa amani na ushirikiano kwa wakazi wa wilaya ya Kyela.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano ya Amani Tanzania JMAT Dkt Sheikh Alhad Mussa Salum amesema kombe hilo limechochea ushirikiano wa kijamii kwa kuwahusisha viongozi wa madhehebu ya dini zote.

Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi- Arusha.

Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha TPF-Net katika kuelekea siku ya wanawake Duniani leo wamefanya ibada maalumu kwa ajili ya kuwaombea Askari Polisi wanandoa waliofariki Dunia kwa ajali ya gari siku mbili baada ya kufunga ndoa.

Akiongea mara baada ya ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Theresia Jijini Arusha Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoani humo Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Happiness Temu amesema mtandao huo umekuwa na utaratibu wa kuyakumbuka makundi mbalimbali yenye uhitaji katika jamii ambapo kwa mwaka huu waliona ni vyema kuwakumbuka Askari waliofariki kwa ajali.

ASP Temu amebainisha kuwa wameamua kufanya Ibada hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwaombea marehemu hao ambao walikua wanafanya nao kazi Mkoani humo kabla kupatwa na umauti Disemba 20, 2022 ambapo pia katika ibada hiyo wamewaombea Watoto wawili ambao waliachwa na marehemu.

Nao baadhi ya askari wa mtaandao huo waliofanya kazi kwa Karibu na marehemu wamebainisha Pamoja na kuwaombea marehemu, pia wametumia ibada hiyo kumshukuru Mungu kwa kuendelea kuwalinda katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande wake Mrakibu wa Polisi SP Asia Matauka ambaye anafanya kazi katika Mkoa wa Kilimanjaro amesema mara baada kusikia juu ya uwepo wa ibada hiyo aliona ni vyema kuungana na mtaandao huo kuwaombea marehemu.

Askari waliofariki na kufanyiwa ibada leo ni Konstebo Noah Simfukwe na Agness Martin.