Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- ZIARA YA NAIBU WAZIRI MAHUNDI ZANZIBAR
- Jinsi ya Kufikisha Malalamiko Kuhusu Mradi wa REGROW na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
- Naibu Waziri Mhandisi Maryprisca Mahundi Akagua Hali ya Mawasiliano Kisiwani Kojani, Pemba
- Inauma sana: Mtoto wangu kaenda chuo kikukuu katumbukia katika umalaya na dawa za kulevya
- WALIOKUWA WANAENDA KUMZIKA NEEMA ALIYEFIA KARIAKOO WAPATA AJALI, MMOJA AJARIKI
- Mbunge Jimbo la Busokelo Mh Mwakibete Serikali ya chama cha Mapinduzi imeitendea haki mkoa wa Mbeya
- Mbunge wa Kyela Ally Jumbe Kinanasi Awakumbusha wana Mbeya
- Mhe. Bahati Ndingo. Uvungu kwa uvungu kitanda kwa kitanda ili Mbarali iendelee kuwa chini ya CCM
Browsing: Video Mpya
HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YAENDELEA KUWA KITUO CHA MFANO KATIKA USIMAMIZI WA UBORA WA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
Katika jitihada za kuendelea kuboresha huduma chini ya Wizara ya afya nchini, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imeendelea kuwa miongoni mwa vituo vya mfano katika umahiri wa usimamizi wa utoaji wa huduma za afya kwa wananchi kupitia mpango maalumu wa usimamizi wa utoaji wa huduma bora katika maeneo ya kazi ujulikanao kama (5S – KAIZEN).
Akiongea baada ya kupokea ujumbe wa wataalam kutoka Wizara ya Afya ulioambatana na Viongozi kutoka nchi mbalimbali waliofika hospitalini hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji amesema lengo kubwa la ugeni huo ni kujifunza na kujionea mpango maalum wa usimamizi wa utoaji wa huduma bora za afya ujulikanao kama (5S – KAIZEN) unatekelezwa na kusimamiwa na kitengo cha Ubora Hospitalini hapa.
“…tumepokea wageni kutoka Wizara ya Afya ya nchi ya Zimbabwe waliokuja hospitalini hapa kujifunza masuala yote yanayohusiana na ubora wa huduma na namna ya kuboresha mambo mbalimbali katika Hospitali.” – Dkt. Godlove Mbwanji
Aidha Dkt. Mbwanji amesema kama hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wamejipanga kuendelea kuboresha huduma kupitia mpango huo, na kutoa wito kwa nchi mbalimbali kuendelea kutembelea hospitalini hapa kujifunza hasa masuala ya utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi kupitia mpango huo wa (5S – KAIZEN)
“…tumejipanga kuhakikisha tunaboresha utoaji wa huduma na tunatoa wito kwa nchi mbalimbali kuendelea kuja kujifunza masuala ya ubora na huduma kwa ujumla.” – Dkt. Godlove Mbwanji
Kwa upande wake mratibu ubora wa huduma kutoka Wizara ya Afya nchini Dkt. Anjelina Sijaona amesema kupitia mpango huo maalumu wa usimamizi wa utoaji wa huduma bora chini ya mradi wa “JAICA” nchini wamepewa nafasi ya kuwa kituo cha mfano wa kutoa mafunzo ya jinsi ya kutumia falsafa ya matumizi ya mpango maalumu wa kuboresha huduma wa “5s – KAIZEN”
“…tumepewa nafasi ya kuwa nchi ya kuonyesha umahili wa jinsi ya kutumia falsafa ya “5S – KAIZEN” katika kuboresha huduma kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka huu na kufanikiwa kupokea zaidi ya mataifa 7 kwaajili ya kujifunza.” – Dkt. Anjelina Sijaona
Dkt. Musiwarwo Chilume ni Mkurugenzi wa uhakiki ubora na usalama wa mteja Wizara ya Afya Zimbabwe amesema, wao kama ujumbe wa wataalamu wa afya kutoka Zimbabwe wamejifunza mambo mengi ikiwemo mifumo na falsafa ya usimamizi wa utaoji wa huduma bora za afya kitu ambacho kimepelekea uwepo wa usimamizi mzuri wa majukumu na uongozi bora ndani ya hospitali hii.
“… tumefurahi kwa kipindi tulichukuwepo hapa kwa kuwa tumejifunza mambo mengi chini ya utelekelezaji wa mpango huu wa “5s KAIZEN” hospitalini hapa uliopelekea uboreshaji wa utoaji wa huduma bora kwa wananchi.” – Dkt. Musiwarwo Chilume
SENETI MKOA WA WA MBEYA WAMUOMBA MWENYEKIT KUWASIMAMIA MIKOPO INAYOTOLEWA NA JIJI.
Hayo ameyasema katibu wa seneti wa chama cha mapinduzi walipokuwa wamekutana viongozi wa chama cha mapinduzi jumuhiya ya vijana vyuo na vyuo vikuu na kumuomba mwenyekiti wa Ccm koa kuwasaidia suala hilo
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Mbarak Alhaj Batenga ameendesha pikipiki kwa lengo la kuwahamasisha waendesha bodaboda kujitokeza kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Sharif Abdul Afisa Mwandamizi kitengo cha mahusiano Jamii na ujirani mwema hifadhi ya Taifa Ruaha amesema kupitia mradi wa REGROW wameandaa Muongozo rafiki wa kupokea na kushughulikia malalamiko kutoka kwa wananchi wanaozunguka hifadhi.
Amesema kupitia mradi wa REGROW viongozi na kamati za kushughulikia malalamiko kuanzia ngazi ya Kijiji mpaka mkoa wamejengewa uwezo kwa kupewa elimu namna ya kutumia muongozo huo ili kupokea na kushughulikia malalamiko ya wananchi. Lengo nikuhakikisha wananchi wanaoathirika na shughuli za hifadhi au Mradi wa REGROW wanawasilisha malalamiko yao na yanashughulikiwa kwa utaratibu unaofahamika.
Aidha Abdul amewasihi wananchi wenye malalamiko wafike ofisi za Serikali ya Kijiji nakuwasilisha malalamiko yao au wapige simu ya bure moja kwa moja kwa Hifadhi ya Taifa Ruaha namba 0800110801 na Wizara ya Maliasili na Utalii namba 0800110804 endapo lalamiko linahusu Hifadhi au Mradi wa REGROW. Malalamiko yote yatashughulikiwa kwa usiri na mlalamikaji atalindwa na sheria na tararibu za nchi.
Wiki ya huduma kwa Mteja, Mbeya UWSA yaendelea kutoa Elimu kwa Umma kuhusiana na matumizi sahihi ya maji na namna bora ya kutunza na kulinda miundombinu ya maji kwa huduma endelevu