Rais wa chama cha walimu Tanzania CWT Leah Ulaya ameikumusha serikali juu ya upandishwaji wa madaraja kwa walimu kutokana na baadhi ya walimu nchini kukaa kwenye nafasi moja kwa muda mrefu hali ambayo inapunguza ufanisi wa ufanyaji kazi kitaaluma
Rai hiyo imetolewa mala baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa 10 wa Mwaka ukiwahusisha umoja wa maafisa Elimu wa mikoa na Wilaya
Aidha katibu wa chama cha walimu CWT Joseph Msalaba amesema mara baada ya mafunzo wanayo yapata maafisa Elimu katika mkutano huo utakao dumu kwa muda wa siku 5 mafunzo yanayo fanyikia mkoani Mbeya utakuwa na manufaa makubwa yatakayo leta manufaa katika sekta ya Elimu nchini