Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYAUWSA)CPA Kayange amesema Mamlaka yake imetenga siku mbili katika juma kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali.
CPA Kayange amesema mradi wa Hasara na Hanza utahudumia Kata ya Iganzo,Ilemi na Mwasenkwa ambapo wananchi wameaswa kuchangamkia fursa hiyo na kwamba wananchi wanaweza kulipa kidogo kidogo kwa makubaliano maalum.
Kayange amesema mradi umefikia asilimia themanini ambapo mpaka sasa zaidi ya kaya mia moja thelathini zimenufaika na mradi huo.
Hata hivyo amesema maboresho yanayofanywa katika chanzo cha Nzovwe utakaonufaisha wananchi wa Isyesye.
Aidha amesema mradi wa maji mto Kiwira umefikia asilimia thelathini.
Kayange amewaomba wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha utekelezaji wa miradi ambapo mradi wa Kiwira unatarajia kutamatika mwezi Aprili,2025 hivyo kumaliza kabisa tatizo la maji Jiji la Mbeya na Mji wa Mbalizi.