Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya imevuka malengo ya makusanyo mapato ya ndani baada ya kukusanya asilimia mia moja arobaini na mbili ikiwa ni ongezeko la asilimia arobaini na mbili hivyo kuongoza kimkoa.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bosco Mwanginde katika kikao cha Baraza ikiwa ni robo ya tatu.Hayo
Mwanginde amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Tamim Kambona wafanyakazi wa ldara zote na Madiwani kila mmoja kwa nafasi yake.
Mwanginde amewasisitiza watumishi wa Halmashauri pamoja na makusanyo mazuri wazingatie matumizi mazuri ili fedha zirudi kwa wananchi kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya Zahanati,Vituo vya afya,barabara,maji na shule.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Tamim Kambona ameanisha baadhi ya vyanzo vya mapato kuwa ni pamoja na ushuru wa madini pia mazao likiwemo zao la tumbaku.
Aidha amesema mapato mengine yametokana na leseni za biashara ambapo ushirikiano wa watumishi kila ldara umesaidia kuvuka malengo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Mubarak Alhaj Batenga amepongeza hatua iliyofikiwa na Halmashauri na kuwataka waendelee kuongeza bidii ya makusanyo ili waongoze kitaifa.
Batenga ameishauri Halmashauri kutenga eneo la malisho kwa ajili ya wafugaji ili kuongoza migogoro ya wakulima,wachimbaji na wafugaji ambapo ameahidi kushughulikia migogoro yote inayohusu mipaka.
Mwakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Afisa serikali za mitaa Christopher Nyambaza Mbeya ameiponeza Halmashauri kwa makusanyo mazuri na kuwataka wasibweteke bali waongeze bidii zaidi huku akiwataka Madiwani kuhakikisha wanaisimamia vizuri inayotekelezwa na serikali na hicho ndicho kipimo chao kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na wahakikishe miradi yote imekamilika.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chunya Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Nestory Mwita John amesema changamoto kubwa ni uharibifu wa Mazingira unaotokana na ukataji wa miti na uchomaji wa mkaa ambapo Jeshi la Polisi halitosis kuwakakata wote wanaojihusisha na biashara hiyo kinyume cha Sheria.
Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya imevuka malengo ya makusanyo mapato ya ndani baada ya kukusanya asilimia mia moja arobaini na mbili ikiwa ni ongezeko la asilimia arobaini na mbili hivyo kuongoza kimkoa.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bosco Mwanginde katika kikao cha Baraza ikiwa ni robo ya tatu.
Mwanginde amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Tamim Kambona wafanyakazi wa ldara zote na Madiwani kila mmoja kwa nafasi yake.
Mwanginde amewasisitiza watumishi wa Halmashauri pamoja na makusanyo mazuri wazingatie matumizi mazuri ili fedha zirudi kwa wananchi kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya Zahanati,Vituo vya afya,barabara,maji na shule.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Tamim Kambona ameanisha baadhi ya vyanzo vya mapato kuwa ni pamoja na ushuru wa madini pia mazao likiwemo zao la tumbaku.
Aidha amesema mapato mengine yametokana na leseni za biashara ambapo ushirikiano wa watumishi kila ldara umesaidia kuvuka malengo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Mubarak Alhaj Batenga amepongeza hatua iliyofikiwa na Halmashauri na kuwataka waendelee kuongeza bidii ya makusanyo ili waongoze kitaifa.
Batenga ameishauri Halmashauri kutenga eneo la malisho kwa ajili ya wafugaji ili kuongoza migogoro ya wakulima,wachimbaji na wafugaji ambapo ameahidi kushughulikia migogoro yote inayohusu mipaka.
Mwakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Afisa serikali za mitaa Christopher Nyambaza Mbeya ameiponeza Halmashauri kwa makusanyo mazuri na kuwataka wasibweteke bali waongeze bidii zaidi huku akiwataka Madiwani kuhakikisha wanaisimamia vizuri inayotekelezwa na serikali na hicho ndicho kipimo chao kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na wahakikishe miradi yote imekamilika.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chunya Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Nestory Mwita John amesema changamoto kubwa ni uharibifu wa Mazingira unaotokana na ukataji wa miti na uchomaji wa mkaa ambapo Jeshi la Polisi halitosis kuwakakata wote wanaojihusisha na biashara hiyo kinyume cha Sheria.
Pia amesema kuna utoroshaji wa madini ya Dhahabu kunakofanywa na watu wasio waaminifu.
Katika hatua nyingine Nestory Mwita John Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chunya amesema kumekuwa na ongezeko la vifo vinavyotokana na wizi wa kimapenzi hivyo amewataka wanandoa kuzimaliza tofauti zao kwa amani badala ya kujiua au kuua.
Diwani wa Kata ya Chokaa Samwel Komba aliuliza swali la papo kwa papo juu ya ya gharama za kuhifadhi miili ya marehemu kwa siku ambapo hutozwa elfu arobaini kwa siku hivyo akiomba zipunguzwe ziwe elfu ishirini kwa siku ili kuwapunguzia ukali wa maisha wananchi wake.
Akijibu swali hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Tamim Kambona amesema gharama hizo zimewekwa kutokana na gharama kubwa za uendeshaji wa majokofu ya kuhifadhia maiti na kwamba majofu hayo yataendelea kufungwa katika Vituo vya afya kama Makongolosi na Kambikatoto ili kusogeza huduma karibu ya wananchi ambapo awali huduma hiyo ilikuwa inapatikana Mbeya.
Baraza limepitisha maazimio yote katika kabrasha lililokuwa limeandaliwa na kamati zote zikiwemo za uchumi,afya na mazingira.