Mkuu wa Wilaya ya Songwe amefanya kikao na uongozi wa Kampuni ya Mamba Minerals inayowekeza katika uchimbaji wa madini adimu duniani ya Rare Earth Metals kijiji cha Ngwala Wilayani Songwe.Kikao hicho ambacho pia kimehudhuriwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Songwe, ndugu Godfrey Kawacha kimefanyika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya zilizopo Mkwajuni.Akizungumza baada ya Kikao hicho, Mhe. Itunda amesema kuwa uongozi huo umemweleza maendeleo ya mchakato wa tathmini na mipango ya kuanza kulipa fidia kwa wananchi.Mkuu huyo wa Wilaya ameusisitiza uongozi huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kwa kila hatua wanayofikia ili wananchi wajue kinachoendelea katika eneo hilo.Pia, DC Itunda amesema kuwa uongozi huo umemweleza kuwa ujenzi wa mgodi huo utaanza Januari, 2025.“Tumefanya kikao na wenzetu wa Mamba, Kampuni ambayo inayowekeza katika uchimbaji wa madini adimu duniani ya Rare Earth Metals kule Ngwala. Kampuni hii wanaanza ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondary Ngwala na Kituo cha Polisi kule Ngwala” amesema DC Itunda.Wawakilishi wa Kampuni hiyo wameongozwa na Mkurugenzi wa Mamba Minerals Corporation Limited ( MML), Ismail Diwani.
Trending
- Maajabu ya Kijungu na Daraja la Mungu
- Gesi ya Samadi Bioges yaokoa Mazingira Rungwe
- Umuhimu wa Sheria ndogondogoza ulinzi wa Mtoto,
- ZAIDI YA WASHIRIKI 3,000 WASHIRIKI UZINDUZI WA KAMPENI YA TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA ARUSHA
- Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Mhe. DoorMohamed Issa: Wana Mbeya Tuendelee kumuunga mkono Dkt Tulia
- TARURA MKOA WA DODOMA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII
- Dkt. Tulia aipongeza Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.
- TARURA YAKAMILISHA UJENZI WA DARAJA LA MSADYA, MKOMBOZI KWA WANANCHI WA MPIMBWE