JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani limeshikilia dreva wa kampuni ya Ahmed Trans lenye namba za Usajili T586 AJH linalofanya safari ya kusafirisha abiria kati ya Mbeya na Tanga Rajab Omari baada ya kumkuta amelewa chakali huku akiwa amebeba abiria tayari ya kwa safari ya kutoka Mbeya kwenda Tanga.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mbeya Mkuu wa Oparesheni ya Trafic kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ACP Nassor Sisiwah amesema wakiwa katika zoezi la ukaguzi wamemkamata Dereva huyo na baada ya kumpima wamemkuta na kileva 450 .3 ml/gm kinyume cha sheria.
ACP Nassor Sisiwah amesema zoezi hilo limelenga pia kufanya ukaguzi wawa magari ambayo yanadaiwa fedha ya Serikali na zoezi litakuwa endelea lakini pia kuwakumbusha wernye vyombo kulipa madeni.
Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya SP Hussen Gawile amesema zoezi ni utaratibu wa kawaida wa Jeshi hilo kufanya ukaguzi ili kuhakikisha wananchi wanakuwa salama wakati wote
Rajabu Ghuliku Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani amesema ukaguzi huo unaonyesha ni jinsi gani Serikali ipo kazini wakati wote huku Dereva Rajab Omary akikiri kuwa amefanya kosa na kwamba hakuwa kwenye ratiba ya safari kwa siku ya leo hivyo amekurupushwa na bosi.