Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameishukuru Serikali kwa kusikiliza kilio cha Wananchi wa Mbeya kwa hatua ya kuanza kuboresha miundombinu mbalimbali katika Jiji la Mbeya ikiwemo barabara ambazo zimekuwa kero kwa miaka mingi.Dkt. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 27 Julai, 2024 wakati wa hafla ya utiaji saini Mikataba ya miradi ya TACTIC ujenzi wa barabara, Kituo Kikuu cha Mabasi na Soko Kuu la Jiji hilo iliyofanyika katika Viwanja vya Aiport ya zamani ambapo Mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Mohamed Mchengerwa.Ameleza kuwa, pamoja na Jiji hilo kuwa na changamoto nyingi suala la barabara limekuwa kikwazo zaidi kutokana na maeneo mengi kutopitika ikiwemo barabara za mitaa hivyo kurudisha nyuma shughuli za maendeleo kwa Wananchi.Sambamba na hayo, Dkt. Tulia amebainisha kuwa baada ya kutoa kilio hicho cha Wananchi tayari Serikali imekwishaanza kufanyia kazi maeneo mbalimbali kwa kujenga barabara za mitaa kwa kiwango cha lami ikiwemo barabara kuu ya njia nne Igawa-Ifisi.Kwa upande wake Waziri Mchengerwa amesema kuwa Wizara yake imepokea maelekezo mahususi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha inatekeleza maombi yote yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Dkt. Tulia ya kuhakikisha inazitatua changamoto zote zikiwemo za barabara, elimu, afya n.k
Trending
- Betty (Rehema) Fwelefwele Kalala wa Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara, Anatafuta Baba Yake Mzazi Aitwaye Method Kapinga
- DKT. TULIA ASISITIZA UMUHIMU WA USALAMA DUNIANI NA MAENDELEO YA PAMOJA
- AJALI TENA!!! BASI LINGINE LAUA 12 WAKIWEMO WATOTO WAWILI RC HOMERA ATOA TAMKO
- TISA( 9) WAFARIKI KATIKA AJALI YA BASI MBEYA
- LIVE: Kura Mayuma aongea baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu Shinyanga
- Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala yaguswa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hasaan kuendeleza Tiba Asili nchini.
- WAPIGA KURA WAPYA 491,050 KUANDIKISHWA MARA, SIMIYU NA MANYARA
- IDARA YA UHAMIAJI YA MULIKWA MAFUNZO MAREKANI, WASHIRIKI WATOA DIRA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO.