AJALI YA GARI KUGONGA MAGARI MATATU NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI.Ni kwamba mnamo tarehe 16.08.2022 majira ya saa 02:00 asubuhi huko maeneo ya Inyala Pipeline, Kijiji cha Shamwengo, Kata ya Inyala, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya katika barabara ya Mbeya – Njombe, Gari lori lenye namba za usajili T.387 DFJ lenye tela namba T.918 DFE aina ya Dayun likiendeshwa na Dereva MUHSIN GUMBO, Mkazi wa Dar es Salaam mali ya kampuni ya Evarest Frech Ltd likiwa na kontena la mchanga likitokea Mbeya liligonga kwa nyuma Gari T.966 DUQ aina ya Fuso basi mali ya kampuni ya Super Rojas likitokea Mbeya kuelekea Njombe likiendeshwa na ALEX MGIMBA [51] Mkazi wa Jijini Mbeya na kisha kugonga Gari T.836 DRE Mitsubish Benz iliyokuwa ikiendeshwa na NEDIM PREMJI, Mkazi wa Dar es Salaam na kisha kugonga Gari linguine T.342 CHG/T.989 CGS Scania iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika na kusababisha vifo vya watu 19 kati yao wanaume ni 12, wanawake 06 na mtoto 01. Aidha katika ajali hiyo majeruhi ni 10 kati yao wanaume ni 07, wanawake ni 02 na mtoto 01.Chanzo cha ajali ni Gari kufeli breki kwenye eneo lenye mteremko mkali na kisha kugonga magari mengine. Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na Hospitali ya Igawilo. Imetolewa na:Ulrich Matei – SACPKamanda wa Polisi,Mkoa wa Mbeya.
Trending
- WAKAZI MTAA WA KATI SOWETO MBEYA WAINGIA MTAANI WAJITENGENEZEA BARABARA ILIYOHARIBIWA NA MVUA
- WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LINDI, MTWARA, RUVUMA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI
- MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI MIKOA YA MTWARA, LINDI NA RUVUMA YAFUNGULIWA LEO
- DROO YA MASTA BATA YA BENKI YA NMB KUWAPELEKA WATEJA WAKE KULA BATA DUBAI
- Jinsi nilivyoweza kupata mchumba toka nchini Marekani
- MATAPELI CCM WABAINIKA,NI WALE WANAOPITA KUOMBA FEDHA BILA RIDHAA YA CHAMA,WATANGAZIWA KIAMA CHAO
- MH. MAHUNDI VIJANA TUACHE KUTUMIA MITANDAO VIBAYA
- Bosi wangu anang’ang’ania kuzaa mtoto na mke wangu!