Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kutokea mkoa wa Mbeya Charles Mwakipesile amewajia juu baadhi ya watu hususani wapinzani ambao wamekuwa wakitoa maneno ya kejeli dhidi ya maendeleo yaliyoletwa na Rais Samia kwa kipindi cha miaka mitatu tangu achukue kijiti cha kuliongoza Taifa kutoka kwa Rais wa awamu ya tano aliyefariki dunia Dkt John Magufuli.

