Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

SIKIA KILIO CHA WAFUNGWA GEREZA LA RUANDA MBEYA KWA RAIS SAMIA

June 19, 2025

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Azindua Kiwanda cha Kwanza cha Uchenjuaji wa Shaba Nchini Chunya, Mbey

June 19, 2025

WANAFUNZI WAFUNGWA WA GEREZA LA RUANDA MBEYA WAHITIMU MAFUNZO CHUO CHA UFUNDI MAGEREZA

June 18, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • SIKIA KILIO CHA WAFUNGWA GEREZA LA RUANDA MBEYA KWA RAIS SAMIA
  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Azindua Kiwanda cha Kwanza cha Uchenjuaji wa Shaba Nchini Chunya, Mbey
  • WANAFUNZI WAFUNGWA WA GEREZA LA RUANDA MBEYA WAHITIMU MAFUNZO CHUO CHA UFUNDI MAGEREZA
  • WAKAZI KATA YA MAJENGO MBEYA WATANGAZA MITANO TENA KWA DIWANI WAO MAULIDI JAMADARI
  • MAMLAKA MAJI MBEYA YABAINI WIZI MKUBWA WA MAJI ENEO LA MAGEREJINI SOWETO MFUMO WA MITA WAHUJUMIWA
  • T/PRISON YAICHIMBA MKWARA YANGA,MBEYA HAICHOMOKI INAHITAJI ALAMA 3 KUJIKWAMUA KUSHUKA
  • Utekelezaji wa Ilani ya CCM Wampa Heshima Meya Mbeya Kata ya Isanga
  • MAKALA MAALUMU: “Utekelezaji wa Miaka Mitano: Kazi, Matendo na Mafanikio ya Mhe. Mahundi”
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » MALIASILI, MAMBO YA NDANI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KUKUZA UTALII
Utalii na Utamaduni

MALIASILI, MAMBO YA NDANI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KUKUZA UTALII

Mbeya YetuBy Mbeya YetuJanuary 24, 2025Updated:January 24, 2025No Comments0 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) (kushoto) na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism), Zurab Pololikashvili (kulia) na wakisaini Makubaliano ya Tanzania kuwa mwenyeji wa Kongamano la 2 la Kikanda la Utalii wa Vyakula la Shirika la Umoja wa Mataifa (The 2nd UN Tourism Regional Forum on Gastronomy Tourism for Africa) katika Makao Makuu ya Shirika la Utalii Duniani la Umoja wa Mataifa  jijini Madrid, Hispania leo Januari 24,2025.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism), Zurab Pololikashvili na wakionyesha makubaliano waliosaini kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Kongamano la 2 la Kikanda la Utalii wa Vyakula la Shirika la Umoja wa Mataifa katika Makao Makuu ya Shirika la Utalii Duniani la Umoja wa Mataifa  jijini Madrid, Hispania leo Januari 24,2025.

Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism), Zurab Pololikashvili akizungumza katika kikao kati yake na Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) (hayupo pichani) kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika la Utalii Duniani la Umoja wa Mataifa  jijini Madrid, Hispania leo Januari 24,2025

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) akizungumza katika kikao kati yake na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism), Zurab Pololikashvili(hayupo pichani) kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Kongamano la 2 la Kikanda la Utalii wa Vyakula la Shirika la Umoja wa Mataifa, kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika la Utalii Duniani la Umoja wa Mataifa  jijini Madrid, Hispania leo Januari 24,2025.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) katika kikao na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism), Zurab Pololikashvili wakijadili kuhusu namna bora ya kuboresha Kongamano la 2 la Kikanda la Utalii wa Vyakula la Shirika la Umoja wa Mataifa (The 2nd UN Tourism Regional Forum on Gastronomy Tourism for Africa) litakalofanyika nchini Tanzania mwezi Machi,2025, kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika la Utalii Duniani la Umoja wa Mataifa  jijini Madrid, Hispania leo Januari 24,2025.

Na Happiness Shayo-Dodoma

Wizara ya Maliasili na Utalii imetakiwa kushirikiana kwa ukaribu na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kukuza soko la utalii nchini na kurahisisha utoaji wa huduma ya viza kwa watalii.

Hayo yamesemwa leo Januari 14,2025 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mnzava katika kikao kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma.

“Wizara ya Mambo ya Ndani, Uhamiaji na Wizara ya Maliasili na Utalii mshirikiane kuikuza Sekta ya Utalii, tunahitaji mfanye zaidi kuisaidia sekta hii na kama kuna changamoto mkazitatue” Mhe. Mnzava amesisitiza.

Mhe. Mnzava amezitaka Wizara hizo kuoanisha mifumo ya malipo kwa watalii na kuweka mikakati madhubuti ya kutambua masoko muhimu ya watalii na kuwavuta waje nchini sambamba na kurahisisha michakato ya kupata viza kwa watalii hao.

Naye, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) ameiahidi kamati hiyo kwamba Wizara ya Maliasili na Utalii itahakikisha inafanya kazi kwa ukaribu na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhakikisha soko la utalii linakua ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kukuza Sekta ya Utalii nchini.

“Tutahakikisha tunatambua masoko muhimu ya utalii na kuweka mikakati madhubuti ya kuvutia watalii kwa kushirikiana ”Mhe. Chana amesema.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Viongozi na Watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake pamoja na Viongozi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ndani ya Nchi na Uhamiaji.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

WADAU WA UTALII DUNIANI WAVUTIWA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA

March 7, 2024

TALII NA MAMA SAMIA HIFADHI YA TAIFA KITULO

December 19, 2023

RC. HOMERA: Nane Nane ya Hadhi ya kimataifa kufanyika Mbeya 2023

June 27, 2023

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024171

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202482

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202566

DKT. TULIA ATOA MSAADA WA VIPAZA SAUTI MSIKITI WA MASJID BI FATMA NZOVWE JIJINI MBEYA

March 29, 202458
Don't Miss
Video Mpya

SIKIA KILIO CHA WAFUNGWA GEREZA LA RUANDA MBEYA KWA RAIS SAMIA

By Mbeya YetuJune 19, 20250

#mbeyayetutv

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Azindua Kiwanda cha Kwanza cha Uchenjuaji wa Shaba Nchini Chunya, Mbey

June 19, 2025

WANAFUNZI WAFUNGWA WA GEREZA LA RUANDA MBEYA WAHITIMU MAFUNZO CHUO CHA UFUNDI MAGEREZA

June 18, 2025

WAKAZI KATA YA MAJENGO MBEYA WATANGAZA MITANO TENA KWA DIWANI WAO MAULIDI JAMADARI

June 17, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

SIKIA KILIO CHA WAFUNGWA GEREZA LA RUANDA MBEYA KWA RAIS SAMIA

June 19, 2025

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Azindua Kiwanda cha Kwanza cha Uchenjuaji wa Shaba Nchini Chunya, Mbey

June 19, 2025

WANAFUNZI WAFUNGWA WA GEREZA LA RUANDA MBEYA WAHITIMU MAFUNZO CHUO CHA UFUNDI MAGEREZA

June 18, 2025
Most Popular

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024171

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202482

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202566
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.