Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Serikali Kutoa Mafunzo Maalum kwa Waandishi wa Blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

July 10, 2025

ONYO KALI KWA VIBAKA KUTOKA KWA WAMACHINGA SOKO LA JIONI KABWE JIJI LA MBEYA VIBAKA NA WEZI WAUFYATA

July 6, 2025

MNEC: MWASELELA ASIMAMISHA MINONG’ONO YA KISIASA MBEYA MJINI

July 3, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Serikali Kutoa Mafunzo Maalum kwa Waandishi wa Blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
  • ONYO KALI KWA VIBAKA KUTOKA KWA WAMACHINGA SOKO LA JIONI KABWE JIJI LA MBEYA VIBAKA NA WEZI WAUFYATA
  • MNEC: MWASELELA ASIMAMISHA MINONG’ONO YA KISIASA MBEYA MJINI
  • KWA MARA NYINGINE, MHANDISI MAHUNDI AWAPA NEEMA WAGONJWA WA MACHO
  • MWAKIPESILE AREJESHA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI
  • Msimu wa pili wa tamasha la michezo na vipaji MZRH
  • MKULIMA NA MFUGAJI WA MBARALI ATIA TIMU KIPUTE JIMBO LA MBARALI USANGU ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE
  • WAKILI MSOMI KAPTENI MSTAAFU SAMBWEE SHITAMBALA ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI.
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » MAPATO MANISPAA YA MOSHI “YAPAA” KUTOKA BILIONI 6.1 HADI BILIONI 9.9
Habari za Kitaifa

MAPATO MANISPAA YA MOSHI “YAPAA” KUTOKA BILIONI 6.1 HADI BILIONI 9.9

Mbeya YetuBy Mbeya YetuFebruary 17, 20251 Comment0 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Zuberi Kidumo akitangaza ongezeko la mapato ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi .
Mkurugenzi wa Hlamshauri ya Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe akizungumza wakati wa baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi .
Baadhi ya Wakuu wa Divisheni na watendaji katika ofisi za Halmashauri ya Manipaa ya Moshi wakifuatilia kikao cha Bajeti cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo.

Baadhi ya Madiwa wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakichangia mjdala wa Bajeti ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakati wa kikao cha Bajeti .

 Na Dixon Hussein – Moshi  

Manispaa ya Moshi imepiga hatua kubwa
katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, ikiongeza mapato kutoka bilioni 6.1 mwaka
2021 hadi bilioni 9.9 mwaka 2025, ongezeko la takribani bilioni 3.7.

Mafanikio haya yanatajwa kuwa matokeo ya mikakati madhubuti
iliyowekwa ili kuboresha vyanzo vya mapato na kuongeza uwajibikaji katika
usimamizi wa rasilimali za umma.

Akizungumza katika kikao cha bajeti cha mwaka wa fedha
2025/26, Meya wa Manispaa ya Moshi Zuberi Kidumo amesema kuwa ongezeko hilo
limechangiwa na mbinu mpya za ukusanyaji wa mapato pamoja na uwekezaji katika
miradi yenye tija.

“Tumeimarisha mifumo yetu ya ukusanyaji wa mapato kwa
kutumia teknolojia ya kisasa, tumeongeza uwazi katika makusanyo, na pia
tumewekeza katika miradi inayozalisha kipato kwa manispaa. Hatua hizi
zimechangia ongezeko kubwa la mapato,” alisema Zuberi Kidumo .

Alisema miongoni mwa mikakati iliyochangia ongezeko la
mapato ni matumizi ya Mfumo wa Kidigitali katika Ukusanyaji wa Mapato na kwamba
mifumo hiyo imepunguza upotevu wa mapato
na kuongeza uwazi.

“Mfumo huu umesaidia kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato
yanayotokana na malipo ya moja kwa moja bila kufuata taratibu sahihi” alisema
Kidumo

Akiwasilisha hoja kwa wajumbe wa baraza la Halmashauri ya Manispaa
ya Moshi Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo Mwajuma Nasombe amesema ofisi
yake kwa sasa imewekeza kwenye miradi mitatu ya kimkakatai .

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ni ujenzi wa vibanda
vingi vya biashara katika eneo la Uhuru Park ,Ujenzi wa bustani na kumbi za nje
kwa ajili ya sherehe kwa maharusi pamoja na ukarabati mkubwa wa uwanja wa
michezo wa Majengo .

Mkurugenzi Nasombe anasema Manispaa imeanzisha mfumo wa
ukaguzi wa mara kwa mara kuhakikisha kuwa mapato yanayokusanywa yanafika kwenye
mfuko wa manispaa bila upotevu huku usimamizi mzuri wa rasilimali na
uwajibikaji wa watendaji umeimarishwa ili kuhakikisha kila senti inayokusanywa
inatumika kwa maendeleo ya wananchi.

Aidha ameeleza kuwa kumekuwa na ushirikiano mzuri na  na taasisi mbalimbali za maendeleo,
wafanyabiashara, na mashirika ya kimataifa katika kutafuta njia bora za
kuongeza mapato na kuwekeza katika miradi mipya.

Mafanikio haya yameifanya Manispaa ya Moshi kuwa mfano wa
kuigwa katika usimamizi wa fedha za umma, huku kukiwa na matumaini makubwa kuwa
mapato yataendelea kuongezeka.

Hata hivyo, changamoto kama ukwepaji wa kodi na uhaba wa
baadhi ya miundombinu bado zinahitaji suluhisho la haraka.

Baadhi ya wananchi wamesifu juhudi za manispaa lakini
wakatoa wito wa uwazi zaidi katika matumizi ya mapato hayo.

“Tunafurahia kuona mapato yanaongezeka, lakini
tunahitaji kuona miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa kasi ili wananchi waone
matunda ya mapato haya,” alisema mkazi mmoja wa Moshi”.alisema Idrisa Mombo
mkazi wa manispaa ya Moshi

Kwa ongezeko hili la mapato, Manispaa ya Moshi inaonekana
kuwa na dira thabiti ya maendeleo. Swali linalosalia ni je, mapato haya
yataweza kuendelea kuongezeka kwa miaka ijayo na kubadili kabisa taswira ya
kiuchumi ya manispaa?

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

Serikali Kutoa Mafunzo Maalum kwa Waandishi wa Blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

July 10, 2025

MHASIBU SUA AJITOSA UBUNGE JIMBO LA SAME MASHARIKI

June 28, 2025

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO WANOLEWA

June 22, 2025

1 Comment

  1. 🔗 + 1.518878 BTC.GET - https://graph.org/Binance-04-15?hs=00df76676ae787764fc48c7ceff27b5a& 🔗 on April 22, 2025 3:27 pm

    nk0pl2

    Reply

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024174

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202483

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202569

DKT. TULIA ATOA MSAADA WA VIPAZA SAUTI MSIKITI WA MASJID BI FATMA NZOVWE JIJINI MBEYA

March 29, 202460
Don't Miss

Serikali Kutoa Mafunzo Maalum kwa Waandishi wa Blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

By Mbeya YetuJuly 10, 202520

Na Mwandishi Wetu Serikali imekubali kutoa mafunzo maalum kwa waandishi wa blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu…

ONYO KALI KWA VIBAKA KUTOKA KWA WAMACHINGA SOKO LA JIONI KABWE JIJI LA MBEYA VIBAKA NA WEZI WAUFYATA

July 6, 2025

MNEC: MWASELELA ASIMAMISHA MINONG’ONO YA KISIASA MBEYA MJINI

July 3, 2025

KWA MARA NYINGINE, MHANDISI MAHUNDI AWAPA NEEMA WAGONJWA WA MACHO

July 1, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Serikali Kutoa Mafunzo Maalum kwa Waandishi wa Blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

July 10, 2025

ONYO KALI KWA VIBAKA KUTOKA KWA WAMACHINGA SOKO LA JIONI KABWE JIJI LA MBEYA VIBAKA NA WEZI WAUFYATA

July 6, 2025

MNEC: MWASELELA ASIMAMISHA MINONG’ONO YA KISIASA MBEYA MJINI

July 3, 2025
Most Popular

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024174

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202483

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202569
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.