Umoja wa Machinga wa eneo la Old Airport katika Jiji la Mbeya wamemchangia Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson, kiasi cha shilingi milioni moja (1,000,000/=) ili aweze kuchukua fomu ya kugombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kufuatia chama hicho kutangaza tarehe rasmi za kuchukua fomu.
Fedha hizo zimekabidhiwa kwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Dormohamed Issa, ambaye alimwakilisha Dkt. Tulia katika hafla hiyo ya makabidhiano.