Wakati ndoa yangu ilianza kuyumba, nilihisi kama dunia imenigeuka na kuanza kunikandamiza. Mume wangu, ambaye zamani alikuwa rafiki yangu wa karibu, mshauri wangu na mtu wa kwanza kumweleza siri zangu, alianza kubadilika taratibu.
Mara alianza kurudi nyumbani usiku wa manane, simu yake akaanza kuweka kwa vibration na kuibeba kila mahali. Nilipomuuliza kwa upole, alinijibu kwa hasira kana kwamba mimi ndiye nilikuwa tatizo.
Nilihisi uchungu mwingi hasa nilipogundua alikuwa na mpango wa kando. Nilipata mshtuko na nilipoteza nguvu za kuendelea na maisha kawaida. Nilianza kukosa usingizi, nilikonda ghafla na hata jirani zangu waligundua kuna jambo baya linaendelea.
Kila nilichojaribu kilionekana kupotea bure. Nilijaribu kuzungumza naye kwa upole, kumshirikisha familia zetu ili watushauri, hata nilijitahidi kusali kila usiku nikiomba mabadiliko, lakini hali ilizidi kuwa mbaya.
Alizidi kuwa mbali nami kiakili na kihisia, na nilijiona kama mgeni ndani ya nyumba yangu mwenyewe. Nilianza hata kufikiria kuondoka, lakini moyoni nilijua singeweza kuvunja familia kwa sababu ya mwanamke wa nje. Nilimwangalia mtoto wangu na nilijua lazima nipambane hadi mwisho kuokoa ndoa yangu. Soma zaidi hapa