Siku hiyo bado naikumbuka kama jana. Nilikuwa nimefungua duka langu mapema kama kawaida, lakini mchana ulipofika nilipokea simu kwamba moto mkubwa ulikuwa umezuka sokoni. Nilipofika pale nilikuta kila kitu kikiwa kimeungua bidhaa, mashine na hata hesabu zangu.

Nilisimama pale nikiwa na machozi, nikishuhudia ndoto yangu ikigeuka majivu. Nilikuwa nimewekeza kila kitu nilichokuwa nacho, na ghafla nilikuwa sina chochote.
Wiki zilizofuata zilikuwa ndizo ngumu zaidi maishani mwangu. Nililazimika kurudi kuishi na ndugu zangu kwa muda kwa sababu nilishindwa hata kulipa kodi ya nyumba yangu.
Nilipitia unyanyapaa kutoka kwa marafiki na majirani waliodhani nisingeweza kuinuka tena. Kila usiku nililala nikiwaza nianzie wapi. Wengi walinipa moyo wa kuanza upya, lakini sikuwa na mtaji wala hamasa ya kufanya chochote. Soma zaidi hapa

 
		 
									 
					